Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko SERIKALI yaitaka Costech kufanya mapitio ya sheria
Habari Mchanganyiko

SERIKALI yaitaka Costech kufanya mapitio ya sheria

Spread the love

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imetakiwa kufanya mapitio ya sheria na sera zilizopo ili kuhakikisha bunifu zinazozalishwa nchini zinatatua changamoto zilizopo ndani ya jamii. Anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 12 Julai, 2022  na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga alipotembelea banda la Costech katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema wakati sheria Na.7 ya mwaka 1986 iliyoanzisha Tume hiyo ikianza kutumika, hapakuwa kifungu kinachozungumzia ubunifu ndani yake, hivyo sasa wanataka kufanya mapitio hayo ili bidhaa zinazobuniwa ziweze kutatua changamoto hapa nchini.

Amesema wamepiga hatua kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kupitia bunifu za ndani  hivyo ni lazima kuhakikisha bunifu hizo zinawanufaisha kwa kutengeneza ajira.

Hata hivyo, Kipanga amesema wameona wabunifu mbalimbali walivyoendelezwa na Costech, kabla ya hapo walikuwa na mfuko wao na pia kuna mashindano yanaitwa makisatu.

“Vyombo vyote hivi vimeundwa kuhakikisha kwamba bunifu pamoja na tafiti zinaweza kukuzwa na kuendelezwa ili badae ziwe bidhaa,” amesema Kipanga

Kipanga ametoa rai kwa Costech kuendelea kufanya kazi na kushirikiana kwa sababu Taifa litajengwa na watanzania wenyewe na lengo la bunifu hizi ni kuhakikisha zinatatua changamoto.

“Tutatumia bunifu zetu za ndani kwa sababu ni rahisi kupata bidhaa inayoweza kutatua changamoto kwa bei rahisi na pia inaweza kutumika kwa urahisi,”amesema Kipanga.

1 Comment

  • Kwa nini kila kitu ni TUTArekebisha.
    Kwa nini isiwe TUMErekebisha.
    Pia lazima mlinde hatimiliki ibakie Tanzania na wazawa. Yule kijana wa mita ya maji aliuza kwa Waingereza sasa hana chochote! Na Waingereza watatuuzia kwa bei yao. Hii tume ilikuwa wapi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!