Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya Exim yakabidhi madawati 100 Tabora
Habari Mchanganyiko

Benki ya Exim yakabidhi madawati 100 Tabora

Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imekabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 mkoani Tabora ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kutoa msaada wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuchangia utoaji wa elimu bora kupitia mpango wake wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ujulikanao kama Exim Cares. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Exim, Zainabu Nungu kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dk.Batilda Buriani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa huyo Mkoa mapema leo tarehe 12 Julai, 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dk.Batilda Buriani (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akipokea msaada wa madawati 100 kutoka kutoka benki ya Exim Tanzania katika kusaidia jitihada za mkoa huo kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Exim, Zainabu Nungu

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wengine waandamizi wa Mkoa huo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Dkt. Yahaya Nawanda, Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Solomon Kasaba, Afisa Elimu Mkoa wa Tabora, Juma Kaponda, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Tabora, Nyahori Mahumbwe, Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Tabora, Joel Mkuchika na wadau wengine wa elimu.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Balozi Buriani pamoja na kuishukuru benki ya Exim kwa kutoa msaada huo, alisema msaada huo unakwenda sambamba na jitihada za serikali za kuboresha hali ya elimu mkoani humo na kwamba msaada huo utasaidia kupunguza uhitaji wa madawati uliotokana na miradi mingi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dk. Batilda Buriani (kushoto) akizungumza na maofisa wa benki ya Exim Tanzania wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Exim Bi Zainabu Nungu (wa pili kulia) wakati maofisa hao walipotembelea ofisi ya mkuu wa mkoa huyo ili kukabidhi msaada wa madawati 100

“Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika baadhi ya shule zetu…tunashukuru sana wenzetu wa Benki ya Exim kwa msaada huu na tunaomba muendelee kusaidia kwenye maeneo mengine pia ikiwemo sekta ya afya. Mheshimiwa Rais anapambana kutafuta fedha kwa ajili ya miradi mikubwa inayoendelea nchini hivyo ni jambo linalotia moyo kwake kuona wadau kama mabenki mkiendelea kumuunga mkono,” alisema.

Aidha Balozi Buriani alizitaja baadhi ya shule zitakazonifaika na msaada huo kuwa ni baadhi ya shule zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ambazo zinazokabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati.

Kwa upande wake Zainabu Nungu alisema kuwa benki hiyo imejitolea kusaidia katika kuboresha ustawi wa jamii kupitia misaada ya kijamii ikiwemo elimu na kwamba wameguswa sana na suala la changamoto ya madawati kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini, sababu iliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo ili kuboresha zaidi sekta hiyo muhimu.

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Exim, Zainabu Nungu (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akikabidhi msaada wa madawati 100 kutoka kutoka benki hiyo katika kusaidia jitihada za mkoa wa Tabora kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt.Batilda Buriani na Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Dk. Yahaya Nawanda (Kushoto)

“Ni furaha kwetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto kwenye sekta muhimu kama hii. Huu ni mwendelezo tu bado tunaendelea na mikoa mingine kwa kuwa lengo ni kutoa msaada wa madawati 1000 kama tulivyoahidi wakati tunazindua mpango huu mwishoni mwa mwaka jana,’’ alisema Bi Zainabu Nungu huku akiitaja mikoa mingine ambayo imekwisha nufaika na mpango huo kuwa ni Dodoma, Mwanza, Lindi, Shinyanga na Mwanza.

Alishauri pia wanafunzi na walimu watakaonufaika na msaada huo kutunza madawati hayo ili yaweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kusaidia walengwa wengi zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!