August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kutimkia Misri, kuweka kambi ya wiki nne

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba inatarajia kuondoka nchini kwenda nchini Miosri kwa ajili ya kufanya maandalizi ya msimu mpya ujao wa mashindano (Pre-Season) katika jiji la Ismailia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kikosi hiko chini ya kocha wao mpya Zoran kitaondoka nchini tarehe 14 Julai 2022, kupitia Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Akitoa taarifa hiyo hii leo, mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam, Meneja wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wachezaji wote ambao wamesajiliwa msimu huu watakuwa sehemu ya safari hiyo huku baadhi yao wakibaki kwa ajili ya majukumu ya Timu ya Taifa.

“Tunatarajia kuondoka na wachezaji wote ambao tumewasajili na tuliokuwa nao msimu uliopita, waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa tutawaacha nyumbani na watajiunga na sisi baadae.” Alisema Meneja huyo

Wachezaji hao wa timu ya Taifa ya Tanzania watakuwa na kibarua tarehe 23 mwezi huu, dhidi ya Somalia katika kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la Matiafa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Aidha Ahmed alisema kuwa kambi hiyo itakuwa ya wiki nne, ambapo wanatarajia kurejea nchii tarehe 5 Agosti 2022, kwa ajili ya maandalizi ya tamasha kubwa la Simba day litakalofanyika Agosti 8, 2022.

“Tunakwenda Misri kwa kuweka kambi ya wiki nne na tutarejea Dar tarehe 5 Agosti mwaka huu, hapo tutakuwa tayari tunekamilisha maandalizi yetu na tukirejea itakuwa ni Simba Day na tutakuwa tayari kwa mchezo wa ngao ya hisani.” Alisema Ahmed

Mchezo huo wa ngao ya hisani utakuwa dhidi ya Yanga, utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Agosti 13 mwaka huu.

error: Content is protected !!