Serikali ya Urusi imewaandalia ushoroba salama wa kupitia wanafunzi wa kitanzania waliokwama Ukrenia katika Chuo cha Taifa cha Sumy ambapo wataondoka kupitia Urusi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Chuo cha Sumy kipo karibu na mpaka wa Ukrenia na Urusi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi leo Machi 5, 2022, wanafunzi watatakiwa kutoka chuoni kuelekea eneo la Sudja ambapo watapoklewa na jeshi la Urusi .
“Kutoka Sudji watasafirshwa na jeshi hilo hadi eneo la Belgorod ambapo watapoklewa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania uliopo Moscow kwa taratibu zingine za kurejea nyumbani Tanzania,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa wanafunzi wanashauriwa kutoka chuoni kwa makundo na kubeba bendera ya Tanzania ili kuwatambulisha wanapopita katika ushoroba huo.
Leave a comment