Wachambuzi wengi wa tukio la uvamizi wa Urusi nchini Ukrenia wamekuwa wakilinganisha ukubwa wa jeshi la Putin na lile la Zelensky. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Kutokana na ukweli kwamba jeshi la Urusi ni kubwa kwa Ukrenia, Waziri wa Ulinzi, Oleskii Reznikov, amesema zaidi ya wanaume wa Ukrenia 66,000 waliokimbia nchi yao awali, wameamua kurejea kuipigania Taifa lao.
Mmoja wa waliorejea ni Yuriy Vernydub (56), ambaye pia ni kocha wa Sheriff Tiraspol iliyoishinda Real Madrid mwaka jana kwenye michuano ya klabu bingwa.
Ameiambia BBC News kuwa ameamua kurejea baada ya kijana wake kumpigia na kumweleza kuwa Urusi wameshambulia.
Leave a comment