Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Rais Samia awapa ujumbe wanafunzi darasa la saba
Elimu

Rais Samia awapa ujumbe wanafunzi darasa la saba

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan amewatakia heri wanafunzi wote wa darasa la saba wanaoanza mitihani yao ya kuhitimu leo Jumatano. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kupitia akaunti yake ya Mtandao X, Rais Samia ameandika; “Mmefikia hatua muhimu ya safari yenu ya awali, kuelekea njia mtakazochagua siku za usoni katika kutoa mchango wenu kusukumu mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa letu.

.”Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu aliyewasimamia toka mwanzo wa safari hii ya elimu hadi sasa, akawape utulivu na afya njema, ili mfanye vizuri mitihani yenu.” ameongeza

Amesma Serikali tayari imekamilisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wote mtakaoendelea na kidato cha kwanza mwaka 2024.

Jumla ya watahiniwa milioni 1.3 wa Tanzania Bara wanatarajia kuanza mtihani wa kumaliza elimu ya msingi waliyoianza miaka saba iliyopita huku wakionywa kuepuka udanganyifu. 

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi (Primary School Leaving Examination PSLE) itafanyika kwa siku mbili kati ya kuanzia tarehe 13 na 14 Septemba 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

Elimu

Vipaji Green Acres vyawafurahisha wazazi

Spread the love WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Green Acres, wamewapagawisha wazazi...

error: Content is protected !!