Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Biashara Serikali yaahidi kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini
Biashara

Serikali yaahidi kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini

Spread the love

SERIKALI imesisitiza kuendelea kupitia upya sera na mfumo wa udhibiti unaoongoza mazingira ya biashara nchini ili kufanya Tanzania kuwa eneo kuu la uwekezaji wa ndani na nje ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza leo Jumatano katika kikao kazi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), Obinna Anyalebechi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, alisema serikali ipo tayari kufanya mazungumzo na sekta binafsi kama njia ya kutatua changamoto zinazokabili wafanyabiashara.

“Sekta binafsi ni mdau muhimu katika ujenzi wa taifa. Tunathamini jukumu la sekta hii katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi, mchango wake katika kutengeneza ajira, ukusanyaji wa mapato ya serikali, na misaada kwa jamii,” alisema Dk. Kijaji.

Katika ziara  iliyofanyika Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL alimshukuru Waziri kwa msaada wake kwa sekta binafsi, jambo ambalo alisema limeongeza hamu na ujasiri wawawekezaji nchini.

Obinna alisema SBL imewekeza zaidi ya Sh bilioni 165 katika miaka mitatu iliyopita kwa lengo la kuongeza uzalishaji wabia na vileo, jambo ambalo limeleta ajira mpya na kuongeza fursa kwa wazalishaji wa ndani kwa kampuni hiyo.

“Upanuzi huu umesababisha kuongezeka kwa uzalishaji na kwa hiyo kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa serikali kutoka kwenye biashara yetu wakati unaimarisha uwezo wa kampuni kufadhili programu za kusaidia jamii zaidi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Programu za kusaidia jamii za SBL, kulingana na Obinna, zinajumuisha utunzaji wa maji, upandaji wa miti, na mafunzo ya stadiza maisha kwa vijana, wanawake, na makundi yanayotengwa.

Kampuni hiyo pia inaendesha programu ya kilimo inayosaidia zaidi yawakulima wa ndani 400 wanaolima shayiri, mahindi, mtama, nanafaka nyingine ambazo kampuni inanunua na kutumia kama malighafi kwa uzalishaji wa bia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

NBC kuchochea ustawi biashara kati ya Tanzania na Afrika kusini.

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake...

Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

error: Content is protected !!