Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Madagascar ajiuzulu ili agombee muhula mwingine
Kimataifa

Rais Madagascar ajiuzulu ili agombee muhula mwingine

Spread the love

RAIS wa Madagascar, Andry Rajoelina amejiuzulu baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais utakaofanyika tarehe 9 Novemba 2023. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, Spika wa Seneti anatakiwa kutwaa mamlaka ya urais katika kipindi hicho cha mpito.

Hatua hiyo ya kujiuzulu kwa rais Rajoelina sio ya kushangaza huko Madagascar kwa sababu ni wajibu wa kikatiba ikiwa rais aliyeko madarakani atawania muhula wa pili ni lazima ajiuzulu kwanza.

Andry Rajoelina, mwenye umri wa miaka 49, alituma barua yake ya kujiuzulu kwa Mahakama siku ya Jumamosi baada ya kuthibitishwa na Mahakama Kuu ya Kikatiba kama mgombea wa urais.

Jambo jipya katika hali hii ni kwamba shughuli zote za kitaifa na majukumu ya rais yataendeshwa na waziri Mkuu kwa pamoja na serikali yake.

Kikatiba Spika wa Seneti ndiye anatakiwa kutwaa mamlaka ya urais wakati mkuu wa nchi anapojiuzulu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mahakama ya katiba ni kwamba Spika wa Seneti, Herimanana Razafimahefa, amekataa kuchukuwa madaraka kwa sababu zake binafsi.

“Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mahakama Kuu ya Madagascar ilichapisha orodha rasmi ya wagombea urais. Kati ya wagombea 28 katika kinyang’anyiro hicho, 13 waliidhinishwa kugombea, akiwemo Andry Rajoelina na marais wawili wa zamani, Marc Ravalomanana na Hery Rajaonarimampianina.

Upinzani umelalamikia mchakato wa maandalizi ya uchaguzi huo akiwamo Masy Goulamaly, mbunge na mgombea wa zamani wa urais ambaye amesema amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huo.

“Kuna hitilafu nyingi katika uchaguzi huu, ugombea wa rais wa sasa unathibitisha hili kwa kushindwa kuheshimu sheria, nadhani ndiyo maana kuna uwezekano wa kutokea mgogoro, hivyo napendelea kujitoa kwenye kinyanganyiro tuone nini kitafuata.”, alisema Goulamaly.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!