Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Museven aagiza muswada wa adhabu ya kifo kwa mashoga ufanyiwe marekebisho
Kimataifa

Rais Museven aagiza muswada wa adhabu ya kifo kwa mashoga ufanyiwe marekebisho

Yoweri Museveni
Spread the love

 

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kutia saini muswada wenye utata  dhidi ya mashoga na wasagaji, ambao umezungumzia adhabu ya kifo katika baadhi ya kesi na kutaka kuwa ni vyema ufanyiwe marekebisho. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, uamuzi wa Museveni ulitangazwa jana Alhamisi jioni baada ya kikao cha wabunge wa chama chake tawala, ambao karibu wote waliunga mkono kuidhinishwa na wabunge mwezi uliopita.

Taarifa zimeongeza kwamba wabunge hao wamekubaliana kuurejesha bungeni ili ufanyiwe marekebisho.
Kwa mujibu wa video iliyorushwa na televisheni ya taifa ya UBC, Museveni anaonekana akipinga ushoga akiwa mji mkuu Kampala, akisema kwamba, “Ulaya imepotea. Wanataka sisi tupotee pia.”

Museveni pia aliwasifu wabunge kwa kupitisha muswada huo, ambao umezua ukosoaji mkubwa wa kimataifa.

1 Comment

  • VIONGOZI WANAOONGOZA KUKOSOA MAAMUZI YA VIONGOZI WENZAO TANZANIA….. KWA MBINU ZOTE TULIZANI HUWA MANAKUBALIANA
    Mwanasiasa maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche ametema cheche kuhusu sakata linaloendelea la Kampuni ya Twiga Cement kutaka kuinunua Kampuni ya Tanga Cement.

    Her Excel. Samia Suluhu

    Mr. Daniel Chongolo

    Mr. Professor Ibrahim Haruna

    Mr. Hamad Masoud Hamad

    Mr. Freeman Aikael Mbowe

    Mr. John John Mnyika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!