Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli awaapisha viongozi aliowateua Ikulu
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli awaapisha viongozi aliowateua Ikulu

Spread the love

RAIS  wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Viongozi hao wameapishwa leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Pia, Rais Magufuli ameshuhudia uapisho wa wakuu wa wilaya za Ilala, Maswa, Kalambo, Rombo na Geita.

          Soma zaidi:

Walioapishwa ni;  Mhandisi Marwa Mwita Bubirya Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe akichukua nafasi ya Christopher Ole Sendeka, Dk. Aloyce Nzuki, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Mhandisi Anthony Sanga, kuwa katibu Mkuu, Wizara ya Maji akichukua nafasi ya Profesa Kitila Mkumbo.

Wengine ni; Dk. Seif Shekilage, kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kuchukua nafasi ya David Kafulila. Dk. Allan Kijazi, Kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Rais Magufuli amemwapisha Mhandisi Nadhifa Kemikimba, kuwa Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Dk. Mwinyi Talib Haji, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!