Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Putin apiga mkwara mataifa ya magharibi
Kimataifa

Putin apiga mkwara mataifa ya magharibi

Spread the love

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin ameyapiga mkwara mzito mataifa ya Magharibi sambamba na Marekani kutokana na kile anachokiita ni malengo ya kutaka kuwagawa wananchi wa Urusi dhidi ya propaganda zao za kutaka kuitawala dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Akihutubia wananchi wake kwa njia ya runinga jana tarehe 16 Machi, 2022 Putin ameonya kuwa harakati za mataifa ya Magharibi na Marekani kutaka kuitawala dunia zinaelekea kufikia ukingoni.

Pia amewaonya matajiri wa Urusi ambao wanaisaliti nchi yao kwa kufuata ushawishi wa mrengo wa Marekani na mataifa ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) ambao amedai wana nia ovu ya kuiangamiza Urusi kwamba hatawaacha salama.

“Sitaki kuwahukumu hao wenye majengo Miami au Ufaransa, ambao wanaishi kwa kula vizuri lakini tatizo ni kwamba wanaishi huko na si huku, ni watu wetu na watu wa Urusi.

“Mataifa ya Magharibi yatajaribu kwa kuwashawishi wasaliti wa nchi yetu, kuigawa nchi yetu, kuwagawa wananchi wetu, kuhangaika kutimiza malengo yao na kuna lengo moja tu kuiangamiza Urusi,” amesema.

Putin amesisitiza kuwa mgogoro uliopo kati yake na Ukraine uliandaliwa mapema kama sababu ya nchi za Magharibi kupata kisingizio cha kuiwekea Urusi vikwazo.

Amesisitiza kuwa nchi hizo hazipendi kuiona Urusi ikiwa imara na yenye uhuru pia ameeleza kuwa mapambano nchini Ukraine yanaendelea vizuri na Urusi itatimiza malengo yake katika vita hiyo.

Aidha, Rais Putin amesema kama mataifa ya Magharibi yanadhani nchi yake itarudi nyuma katika vita hiyo basi ni kwamba hawaielewi vizuri Urusi.

Amedai kwamba vikwazo vya kiuchumi vinavyowekwa na mataifa ya Magharibi havina nguvu kwa sababu mataifa mengi hayaungi mkono vikwazo hivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!