Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watumishi 190,781 wapandishwa vyeo, madaraja
Habari Mchanganyiko

Watumishi 190,781 wapandishwa vyeo, madaraja

Spread the love

SERIKALI imesema ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu jumla ya watumishi wa umma 190,781 wamepandishwa vyeo baada ya kusubiri kwa muda mrefu licha ya kuwa na sifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yameelezwa jana Jumatano tarehe 16 2022 na Waziri wa Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama, akielezea mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani.

Mhagama amesema upandishwaji huo wa vyeo na madaraja umeigharimu Serikali jumla Sh 39 bilioni ndani ya mwaka mmoja.

Aidha, amesema ndani ya mwaka mmoja Rais Samia amelipa malimbikizo ya mishahara kwa watumishi 65,394 ya jumla ya Sh 91.8 bilioni, “ni maamuzi ya kijasiri, maamuzi ya busara na ya kuonyesha namna gani Rais wetu anawapenda watumishi wake.”

Vilevile amesema Rais Samia aliamua kuwabadilisha kada watumishi 19,386 na ubadilishaji huo uligharimu Sh 1.3 bilioni, “ndani ya mwaka mmoja akatekeleza jambo hili la kishujaa kabisa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!