Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB yamwaga mikopo ya Sh1.8 trilioni kwa zaidi ya wanawake 168,000
BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yamwaga mikopo ya Sh1.8 trilioni kwa zaidi ya wanawake 168,000

Spread the love

BENKI ya NMB imetoa zaidi ya Sh1.8 trilioni kwa wanawake 168,600 wa biashara ndogo na za kati (SMEs) katika kipindi cha miezi 10 ndani ya mwaka huu (kuanzia Januari hadi Oktoba) ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo katika kuchochea ukuaji wa uchumi endelevu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

 Pamoja na mambo mengine, mkakati kabambe wa benki hiyo unalenga kuimarisha uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kote nchini.

Afisa Mkuu Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Jukwaa la Kuwezeshaji Wanawake Taifa, Fatma Kange (kushoto) wakati wa mkutano ulioandaliwa na Benki ya NMB na kuwakutanisha wakuu wa taasisi mbalimbali zinazoongozwa na wanawake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Frednand Mpona.

 Akizungumza wakati wa hafla iliyokutanisha baadhi ya viongozi wa benki na uongozi wa vikundi mbalimbali vya wanawake iliyofanyika na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli alisisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kusaidia ushirikishwaji wa kifedha kwa wanawake.

Aliongeza kuwa benki yake inaamini kuwa uwezeshaji wanawake ni chachu ya maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

 “Katika benki ya NMB, tumejidhatiti kuziba pengo la ushirikishwaji wa fedha na tutaendelea kufanyia kazi azma yetu kwa kufikisha huduma za kibenki kwa wasio na benki nchini kote wakiwemo wanawake kupitia falsafa yetu ya karibu yako. Kufikia sasa mwaka huu, tayari tumefungua akaunti milioni 2.3 mwaka huu,” alisima Mejooli.

Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, akitoa mada wakati wa mkutano baina ya Benki ya NMB na Wakuu wa taasisi mbalimbali zinazoongozwa na Wanawake jijini Dar es Salaam.

 Mejooli alisema kama sehemu ya kutimiza dhamira yake ya uwezeshaji wanawake, NMB mwezi Novemba mwaka 2020, ilizindua hati fungani yake ya ‘NMB Jasiri Bond’, jukwaa ambalo linalenga kuwawezesha na kuhamasisha ushirikishwaji wa kifedha kwa wanawake katika sekta mbalimbali si tu Tanzania bali Kusini mwa Jangwa la Sahara.

“Mchakato huu ulilenga kutoa mikopo nafuu kwa biashara zinazoongozwa na wanawake na biashara ambazo zinaathiri wanawake moja kwa moja,” aliongeza

Mejooli alibainisha benki yake itaendelea na kampeni za elimu ya masuala ya fedha nchini kote ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kujenga uwezo kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake.

 

Afisa Mkuu Huduma Shirikishi Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli (katikati) akizungumza na Rais wa Wakandarasi Wanawake Tanzania, Mhandisi Judith Odunga, (kushoto) wakati wa mkutano baina ya Benki ya NMB na Wakuu wa taasisi mbalimbali zinazoongozwa na Wanawake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Frednand Mpona.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutika Benki ya NMB, Alex Mgeni wakati wa hafla hiyo alibainisha kuwa benki hiyo tayari imeanza mipango ya kuanzisha kanzidata ya kitaifa ya wanawake itakayorahisisha utoaji huduma za kibenki kwa wanawake katika sekta mbalimbali.

Mgeni alisema benki yake tayari imeanza kutafakari upya jinsi ya kuendela kushirikiana na wanawake wajasiriamali ili kuwawezesha kuondokana na changamoto za kibiashara kwa kutoa bidhaa zinazotengenezwa na mahitaji mengine muhimu yasiyo ya kifedha ili kuendeleza ukuaji wao.

“Tayari tumeshatambua baadhi ya sekta muhimu na nia yetu ni kuhakikisha kwamba tunawaleta wanawake wote katika kanzidata yetu. Kanzidata hii itahakikisha kwamba tunatoa huduma za kibenki zilizotengenezwa mahususi na kwa wakati kwa wanawake,” Mgeni alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!