Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara Kampuni ya Saruji ‘Holcim Group’ yajiondoa soko la Tanzania
Biashara

Kampuni ya Saruji ‘Holcim Group’ yajiondoa soko la Tanzania

Spread the love

Kampuni kubwa ya Saruji ya Uswizi imetangaza mpango wa kuuza kampuni yake tanzu Pan African Cement, ambayo inashikilia asilimia 65 ya Kampuni ya Saruji Mbeya (Mbeya Cement), kwa Kampuni ya Amsons Group. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua ya kujiondoa katika soko la Tanzania, kulingana na taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki, inalenga kuoanisha mkakati wa Holcim wa 2025, ‘Kuharakisha Ukuaji wa Kijani’ ambao unalenga katika kuimarisha uongozi wake katika masoko ya msingi.

“Kampuni ya Holcim Group imefikia makubaliano na kampuni ya Amsons Industries (T) Ltd ya kuiuzia kampuni yake tanzu ya Pan African Cement Limited, ambayo ina hisa asilimia 65 katika kampuni ya Mbeya Cement,” amesema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Holcim’s Lafarge Tanzania, Medhat Ismail katika taarifa aliyoitoa jana.

Medhat Ismail

Ofisa Mtendaji Mkuu huyo Ismail aliiongeza katika taarifa yake hiyo kuwa mchakato wa kuuza kampuni hiyo tanzu ya Pan African Cement kwenda Kampuni ya Amsons Group, uko katika hatua ya kuidhinishwa na mamlaka husika za serikali.

“Tumefurahi kupata mshirika wa kimkakati na anayeaminika wa biashara huko Amsons Group, ambayo iko katika nafasi nzuri ya kuendelea kuwekeza katika ukuaji wake wa muda mrefu,” aliongeza Ofisa Mtendaji huyo.

Kiwanda hicho cha Mbeya Cement kinadhamani ya dolla za Kimarekani milioni 170, taarifa hiyo ilisema, shughuli za kampuni ya Mbeya Cement zitaendelea bila usumbufu, na kudumisha kasi na viwango vya biashara.

“Holcim inasisitiza ahadi yake kwa wafanyakazi wake wa Mbeya Cement, tunatambua na kuathmaini mchango wao katika ukuaji wa kampuni,” alisema na kuongeza, “Kampuni inathamini kujitolea kwa mnunuzi katika kukuza talanta za ndani na kukuza utamaduni unaohimiza ukuaji na maendeleo.”

Holcim imeyaelezea makubaliano ya mauzo na Amsons Group kama hatua nzuri kwa washikadau wote wanaohusika.

“Inaashiria fursa ya matumaini kwa mustakabali mzuri na wenye faida kwa Mbeya Cement, kuhakikisha mwendelezo na ukuaji wa biashara,” alisema Ismail.

Hivi sasa, Amsons ina ushiriki mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi na bidhaa zilizosindikwa kwa watumiaji katika mataifa ya Tanzania, Msumbiji na Zambia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Biashara

Mchezo wa maokoto Cobra Queen unapatikana Meridianbet

Spread the love Meridianbet Kasino Mtandaoni utapata fursa ya kufurahiamchezo uliochochewa na...

error: Content is protected !!