JUMLA ya wagombea urais 26 wanatarajiwa kuanza kampeni leo Jumatatu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambazo zinatarajiwa kudumu kwa mwezi mmoja na kuhusisha pia wagombea wa nafasi ya ubunge.
Takriban wapiga kura milioni 44 waliojiandikisha, kati ya wakazi karibu milioni 100, watamchagua rais tarehe 20 Desemba 2023. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).
Pia watawachagua kati ya maelfu ya wagombea ubunge na wajumbe wa serikali za mitaa katika nchi hiyo yenye rasilimali nyingi lakini ikiwa imegubikwa na migogoro na ufisadi.
Kampeni ya mapema imekuwa ikiendelea kwa muda, huku Rais Felix Tshisekedi, ambaye anawania muhula wa pili, akihudhuria hafla nyingi za umma akiwa sambamba na washirika wake wanaosifia utendaji katika uongozi wake.
Leave a comment