Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchungaji USA: Watanzania fanyeni kazi, miujiza ya mafuta, maji ni ulaghai
Habari Mchanganyiko

Mchungaji USA: Watanzania fanyeni kazi, miujiza ya mafuta, maji ni ulaghai

Spread the love

JAMII imetakiwa kufanya kazi ambazo zitawaingizia kipato kwa ajili ya kuinua uchumi wao badala ya kujenga fikra ya kupata miujiza kwa kununua udogo, maji au mafuta kutoka kwa manabii. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mchungaji Prof. Livingston Imbuga wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la PAG lililopo Sabasaba Jijini Dodoma katika hafla fupi ya kumtunuku shahada ya uzamivu ya heshima, Mchungaji Charles Kanyika.

Mchungaji Charles Kanyika

Prof. Imbuga ambaye pia ni mwalimu wa Chuo kikuu cha International Universty of Ministry and Education Missouri  cha nchini Marekani, amesema watu wengi wavivu kufanya kazi na hawana uelewa wa kutosha kuhusu neno la Mungu hali inayowalazimu kutegemea zaidi miujiza kutoka kwa manabii ambao kwa kiasi kikubwa ni wachumia tumbo.

Amesema wapo watu ambao wanajiita mitume na manabii ambao wanacheza na akili za watu kuwa kuwauzia vitu ambavyo haviwezi kuwasaidia badala ya kuwafundisha kufanya kazi kwa lengo la kujipatia kipato.

Amesema kuwa mtu hawezi kuwa na uchumi imara kama hafanyi kazi kwa bidii kwani Mungu anaeleza bayana kuwa asiyefanya kazi na asile na kuongeza atabariki kazi za mikono na si kununua udogo au mafuta na maji.

Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la PAG, Dk. Charles Kanyika baada ya kutunukiwa PhD ya heshima ya utatuzi wa migogoro na kuhudumia jamii, amesema kati ya jambo ambalo hakubaliani nalo ni kuona watu wanaonewa au wananyanyaswa.

Amesema kwa kipindi hiki ambacho Tanzanian inaelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025, haki ni lazima itendeke na asiwepo mtu wa kumuonea mwenzake.

Mchungaji Prof. Livingston Imbuga

Amesema ili kuwa na amani ni lazima kuwepo haki na haki pekee ndiyo inayoweza kuzalisha amani  kwa kuwasikiliza wananchi na kuwaacha wachague mtu ambaye wanamuamini.

Aidha, amewataka viongozi wote kwa kada mbalimbali kuhakikisha wanatenda haki huku akiwakumbusha viongozi wa dini kusimama kidete kuhubiri haki, amani na upendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!