Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mambo mazito kwa mchungaji Mackenzie, makaburi mapya yagunduliwa, maiti zafikia 426
Kimataifa

Mambo mazito kwa mchungaji Mackenzie, makaburi mapya yagunduliwa, maiti zafikia 426

Spread the love

KUGUNDULIWA kwa makaburi mapya ya halaiki katika msitu Shakahola huko Kilifi nchini Kenya kumetajwa kuchangia uamuzi wa kurejesha mchakato mpya wa ufukuaji wa makaburi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Makaburi hayo yalianza kugundulika Aprili mwaka huu baada ya Mchungaji Paul Nthenge Mackenzie wa Kanisa lake la Good News International kudaiwa kuwalaghai waumini wake wafunge bila kula ili wakutane na Yesu Kristu.

Awamu ya tano ya zoezi la ufukuaji wa makaburi inatarajia kuanza leo huku taarifa zikieleza kuwa hadi sasa makaburi mapya 40 yametambuliwa.

“Tulirudi kuchora ramani ya makaburi na tumegundua takribani maeneo mapya 40 ya makaburi hadi sasa. Awamu ya tano ya ufukuaji wa makaburi hayo itafanyika kuanzia wiki ijayo,” mmoja wa wapelelezi aliueleza mtandao wa Taifa leo nchini humo.

Lakini, hawakuweza kufichua makadirio ya idadi ya miili katika makaburi hayo ya halaiki yaliyopatikana hivi majuzi kutokana na matatizo yanayotokana na sababu za udongo.

Shughuli hiyo ilisitishwa mwezi Julai ili kupisha uchunguzi wa miili 87 iliyofukuliwa katika awamu ya nne na kufikia Agosti uchunguzi wa maiti ulikamilika wa miili yote iliyofukuliwa katika ya ardhi ya Shakahola.

Kwa mujibu wa Mkuu wa idara ya upasuaji wa Serikali, Dk. Johansen Oduor ambaye aliongoza zoezi la upasuaji wa maiti amesema idadi ya waliofariki ilifikia 426.

Aidha, njaa imeonekana kuwa chanzo kikuu cha vifo katika miili 99, baadhi ya waathiriwa wakiwemo watoto, walinyongwa (14) hadi kufa, au kukosa hewa,

Chanzo cha vifo vya miili 66 hakikubainika katika kile Oduor alitaja kuwa miili kuharibika vibaya.

Mmoja wa waathiriwa aliripotiwa kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua, huku wengine watatu wakiugua matatizo kama vile figo kushindwa kufanya kazi.

Wengi wao walifunga hadi kufa kwa madai ya kutaka kuonana na Yesu. Watu hao walizikwa katika shamba kubwa la ekari 800 msituni Shakahola karibu kilomita 70 kutoka Malindi kulingana na mafunzo yaliyoaminiwa kutolewa na mhubiri Paul Mackenzie ambaye hadi sasa anasota gerezani akisubiri kesi yake inayounguruma nchini humo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Malindi (MCHRC), Victor Kaudo ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu na familia za waathiriwa na serikali, hadi sasa vipimo vya msimbojeni (DNA) 125 vimelinganishwa.

Mei mwaka huu, serikali ilizindua mpango wa DNA kwa familia zinazoamini kuwa jamaa zao ni miongoni mwa waliopotea au kupatikana wamekufa katika msitu wa Shakahola eneo la Kilifi.

“Mpango wa kutoa miili kwa familia umepangwa kufanyika kuanzia leo Jumatatu. Wanaotupigia simu tunawaunganisha na serikali ili waamue lini na vipi watavyopokea maiti za watu wao,” alisema Kaudo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!