Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Biashara TPA yajivunia Zimbabwe kuwa soko jipya mizigo ya magari bandari Dar
Biashara

TPA yajivunia Zimbabwe kuwa soko jipya mizigo ya magari bandari Dar

Spread the love

KAMPENI ya kuitangaza bandari ya Dar es Salaam kimataifa imetajwa kuanza kuzaa matunda baada ya wafanyabiashara na wakazi wa Zimbabwe kuichagua bandari hiyo kupitisha mizigo mbalimbali hususani magari. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua hiyo imetajwa kuendelea kuvutia wateja wengi wa kimataifa kuitumia bandari ya Dar es Salaam na kuilazimu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufungua ofisi katika jiji la Harare ili kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wake.

Hayo yamebainishwa wiki iliyopita na Afisa Uhusiano Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Levina Kato wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika mkoani Lindi.

Kati alisema mbali na kampeni iliyofanywa na mamlaka hiyo, baada ya nchi jirani ikiwamo Afrika Kusini ambako Zimbabwe walikuwa wanatumia kupitisha magari yao, wamepitisha sheria ambazo zinaongeza gharama kwa waagizaji magari.

“Walipitisha sheria ya kuzuia magari hayo mapya yasipitishwe kwenye barabara zao hivyo wateja wakawa wanatumia gharama kusafirisha mzigo kupitia car carrier kwa sababu lazima anayepakia magari alipwe.

“Kwa kuwa ni gharama kubwa kwao, wakaamua kuchagua bandari za Tanzania ili wayaendeshe wenyewe magari hayo badala ya kupitia Afrika Kusini na Zambia,” alisema.

Aidha, aliongeza kuwa TPA imeendelea kuboresha bandari mbalimbali nchini ikiwamo Lindi ambako sasa mkandarasi yupo ‘site’ kuboresha bandari ya uvuvi.

Mbali na maboresho hayo kwenda sambamba na bandari ya Mtwara, Kato alisema kwa upande wa Mwanza mamlaka hiyo inaboresha bandari za mkoa huo ili ziweze kuhudumia vema sokola Uganda kupitia eneo maarufu la biashara Port Bell.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

Biashara

Haya ni Maajabu ya sloti ya Jade Valley ya kasino ya mtandaoni Meridianbet

Spread the love  JADE Valley ni mchezo wa sloti wenye nguzo tano...

Biashara

Washindi wa Serengeti Maokoto ndani ya Kizibo Dar, Dodoma walamba mzigo

Spread the love Mustapha Ally, Mkazi wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma...

Biashara

Shinda mtonyo mrefu ukicheza Shaolin Crew kasino ya  Meridianbet

Spread the love  TAIFA la Uchina limebebwa na historia kubwa sana, wengi...

error: Content is protected !!