Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara NBC yafuturisha wateja, yapongezwa kwa ushirikiano
Biashara

NBC yafuturisha wateja, yapongezwa kwa ushirikiano

Spread the love

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeandaa hafla ya futari mahususi kwa wateja wake wa Kiislamu Visiwani Zanzibar ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuandaa hafla za namna hiyo maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuimarisha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hafla hiyo imefanyika jana kwenye hotel ya Madnat Al  Bahr, Zanzibar ikiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar, Zubeir Ali Maulid huku Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, La Riba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi  kwenye hafla.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, La Riba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa (Katikati) akimkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid (kushoto) zawadi maalum wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana Ijumaa visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo viongozi waandamizi serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Wajumbe wa baraza la wawakilishi, wabunge na wateja wa benki hiyo, Spika Zubeir alipongeza benki ya NBC kwa ushirikiano wake na wadau wake huku akisisitiza umuhimu wa mahusiano yanayogusa na kuheshimu misingi ya imani za dini kwa wateja wa benki.

Kwa upande wake Urassa alisisitiza juu ya umuhimu wa uhusiano mzuri kati ya benki na wadau wake muhimu ikiwemo Serikali na wateja.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid akiwaongoza wageni wengine waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC kupata chakula wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Alitumia fursa hiyo kuzungumzia huduma maalum inayotolewa na Benki ya NBC kwa wateja wa Kiislamu inayojulikana kama La Riba, ambayo inazingatia mafundisho ya Kiislamu kuhusu riba.

Hafla hiyo pia ilihusisha utoaji wa zawadi kwa wageni waalikwa. Kwa wateja wa Kiislamu wa benki ya NBC visiwani Zanzibar, hafla hiyo ilikuwa fursa nzuri ya kufurahi pamoja na kujenga uhusiano mzuri miongoni mwao na benki hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Biashara

Mchezo wa maokoto Cobra Queen unapatikana Meridianbet

Spread the love Meridianbet Kasino Mtandaoni utapata fursa ya kufurahiamchezo uliochochewa na...

error: Content is protected !!