Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Odinga avuka kihunzi cha kwanza uenyekiti AUC
Habari za SiasaKimataifa

Odinga avuka kihunzi cha kwanza uenyekiti AUC

Raila Odinga
Spread the love

AZMA ya kiongozi wa Azimio La Umoja-One Kenya, Raila Odinga kuwania wadhifa wa Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Afrika (AUC) imepata nguvu baada ya kikao kilichoketi jana huko jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuondoa kikwazo cha suala la jinsia kwa wagombea. Inaripoti Mitandaoya Kimataifa… (endelea).

Kwenye kikao hicho maalum kilichoandaliwa jana Ijumaa, uamuzi huo uliofikiwa sasa utafanya Odinga kushusha pumzi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mawaziri na Waziri wa Masuala ya Kigeni nchini Kenya, Musalia Mudavadi, alisema kigezo cha kwamba mwenyekiti ajaye wa AU awe mwanamke, limeondolewa.

Vilevile ilikubaliwa katika kikao hicho kwamba mwenyekiti mpya awe ni wa kutoka Afrika Mashariki ingawa ukanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) itaamua yenyewe wagombea watakaojitosa uwanjani.

“Hizi ni habari nzuri kwa eneo la Afrika Mashariki kutoa wagombea wa kiti cha Mwenyekiti wa AUC,” alisema Mudavadi.

Uamuzi huo wa Baraza la AU sasa unasubiri baraka marais na viongozi wa nchi wanachama wa AU.

AU ina wanachama 55 ambao tangu 2021, AU ilikuwa imeafikia makubaliano kwamba Naibu na Mwenyekiti wa AUC wawe wa jinsia tofauti.

Lakini hayakuwepo makubaliano yoyote kwamba jinsia liwe ni suala la kupokezana kutoka kwa Mwenyekiti mmoja hadi mwingine. Kwamba akitoka mwanamume aingie mwanamke.

Mwaka 2018, makubaliano yaliafikiwa kwamba maeneo yawe yakipokezana fursa ya kutoa Mwenyekiti ambapo maeneo yaliorodheshwa kama kanda ya Afrika ya Kati, kanda ya Mashariki, kanda ya Kaskazini, kanda ya Magharibi na kanda ya Kusini.

Mwenyekiti wa sasa wa AUC, Moussa Faki Mahamat anatoka Chad katika kanda ya Afrika ya Kati na naibu wake ni Monique Nsanzabaganwa wa Rwanda katika kanda ya Afrika Mashariki.

Kanda ya Kaskazini ndio pekee itakayotoa wagombea wa kiti cha unaibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!