Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 12 wafanyiwa upasuaji rekebishi wa macho Mloganzila
Habari Mchanganyiko

12 wafanyiwa upasuaji rekebishi wa macho Mloganzila

Madaktari bingwa wa macho, Nabila Elias, Safwat El Badri kutoka Sudan kwa kushiriiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Kanda ya Mbeya, Tumbi Kibaha, Benjamin Mkapa ya Dodoma , Ligula Mtwara na St. Benedict ya Lindi wakifanya upasuaji rekebishi wa macho kwenye hospitali ya Mloganzila wakati wa kambi maalum ya siku tano
Spread the love

WATU 12 wamefanyiwa upasuaji rekebishi wa macho kwenye kambi ya macho iliyoendeshwa na Hospitali Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na taasisi ya utalii tiba ya Global Medicare. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kambi hiyo ilifanywa na madaktari bingwa wa macho, Nabila Elias, Safwat El Badri kutoka Sudan kwa kushiriiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Kanda ya  Mbeya, Tumbi Kibaha, Benjamin Mkapa ya Dodoma , Ligula Mtwara na St. Benedict ya Lindi.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Naibu  Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili tawi la Mloganzila, Dk Eric Muhumba, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuhitimishwa kwa kambi hiyo.

Alisema waliamua kuwashirikisha madaktari bingwa wa ndani ili kupata ujuzi huo ambao haupatikani hapa nchini kwani wagonjwa wamekuwa wakisafiri kwenda kupata huduma hiyo nje ya nchi.

Madaktari bingwa wa macho, Nabila Elias, Safwat El Badri kutoka Sudan kwa kushiriiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Kanda ya Mbeya, Tumbi Kibaha, Benjamin Mkapa ya Dodoma , Ligula Mtwara na St. Benedict ya Lindi wakifanya upasuaji rekebishi wa macho kwenye hospitali ya Mloganzila wakati wa kambi maalum ya siku tano

Alisema kambi hiyo maalumu ya upasuaji rekebishi wa macho ilihusisha watu wenye uvimbe nje ya jicho, makengeza kwa watu wazima, majeraha yatokanayo na ajali au makovu ya muda mrefu ya macho na wagonjwa wengine  wanaotoka machozi kwa muda mrefu kutokana na kuziba kwa njia za machozi.

Alisema upasuaji huo umefanyika kwa kiwango kikubwa bila changamoto zozote na wagonjwa wanaendelea na maisha yao kama kawaida.

Alisema watu 50 walifika kwenye kambi hiyo kwaajili ya kupata huduma hiyo lakini waliofanikiwa kufanyiwa upasuaji rekebishi ni wagonjwa 12 pekee.

Daktari bingwa wa macho kutoka hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya, Stephane Nyamsanya, aliishukuru hospitali ya Mloganzila kwa kuwaalika kuja kushiriki upasuaji huo wa aina yake.

“Kuna mambo tumeshuhudia tulikuwa tunayafahamu lakini mengine mengi hatukuwa tunayafahamu kwa hiyo tumepata ujuzi na tumejengewa ujuzi ili tuweze kuwatibu wagonjwa wa aina hii hapa nchini na wasilazimike tenda kwenda nje ya nchi,” alisema

Naye Catherine Makunja, ambaye ni daktari bingwa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, alisema hospitali hiyo imekuwa ikitoa matibabu ya ubingwa bobezi kwa matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini.

Alisema hali hiyo imesaidia kuwapunguzia wananchi adha ya kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hizo na kwamba miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na huduma ya kupunguza uzito kwa puto maalum, upasuaji wa kupunguza uzito na upandikizaji wa figo kwa kuvuna figo kwa kutumia matundu madogo.

Alisema hospitali hiyo pia imekuwa ikitoa uvimbe kwenye ubongo kwa kutumia tundu dogo.

Msemaji wa Global Medicare, Albert Kilalah, alisema kambi hiyo inakuja kufuatia uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba vilivyonunuliwa na serikali ya awamu ya sita samabamba na madaktari kusomeshwa kwa wingi na kupewa utaalamu wa hali ya juu kufanya matibabu ya kibingwa.

Alisema zamani matibabu kama hayo yalikuwa yakifanyika nje ya nchi lakini kutokana na uwekezaji huo matibabu hayo yanafanyika hapahapa nchini.

“Zamani wagonjwa kama hawa tuliwapeleka nje ya nchi, lakini sasa madaktati bingwa kutoka nje wanakuja kuwatibu wagonjwa wetu hapahapa kwasababu nchi ina kila aina ya vifaa tiba ambavyo tulikuwa tunalazimika kuvifuata  nje ya nchi na kwa sasa nchi ina madaktati bingwa wenye uwezo mkubwa wa kutumia vifaa hivyo,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!