Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateua, amtumbua Kamishna Ngorongoro
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ateua, amtumbua Kamishna Ngorongoro

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya
uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali ikiwamo utenguzi Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Richard Rwanyakaato Kiza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kiza ambaye awali alikuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),tarehe 12 Oktoba mwaka jana aliteuliwa na Samia kuwa Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunusi ni kwamba Rais Samia amemteua Ally Senga Gugu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu, Gugu alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

Pia amemteua Kaspar Kaspar Mmuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huu Mmuya alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Taarifa imeeleza pia kuwa Rais Samia amemteua Mhandisi Mwajuma Waziri kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Kabla ya uleuzi huu Mhandisi Waziri alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Mhandisi Waziri anachukua nafasi ya Prof. Jamal Katundu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia amemteua Ephraim Mafuru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mafuru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Mafuru anachukua nafasi ya Damasi Mfugale ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!