Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RPC Muliro azindua huduma ya taxi mtandaoni
Habari Mchanganyiko

RPC Muliro azindua huduma ya taxi mtandaoni

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amezitaka kampuni za usafiri mtandaoni kuajiri vijana wenye sifa ya kudadisi abiria wanaowabeba kwa maswali yenye mwelekeo wa kutambua masuala ya usalama. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Aliyasema hayo  leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya taxi mtandaoni maarufu kama SUKA.

Muliro alisema kampuni zinazotoa huduma za usafiri mtandaoni ni mdau muhimu sana kwa serikali kwa masuala yanayohusu usalama kwani wanahudumia watu wengi tofauti.

“Unapoingia kwenye kutoa huduma kama hii automatically wewe ni wakala wa serikali lazima uwe mdadidi siyo kwa maswali yenye maudhi lakini maswali yenye mwelekeo wa kutambua masuala ya usalama,” alisema

Alisema kuna Kampuni zilizokuwa zinatoa huduma zinazofanana na SUKA  hivyo kuwataka wamiliki wa kampuni hiyo kufuatilia kujua walifanikiwa kwa kiwango gani na walikwama wapi wakati wa kufanya shughuli zao.

“Fuatilieni mjue kumbukumbu za kampuni hizo zikoje kwenye mamlaka zilizofanya usajili wake na wananchi ambao walikuwa wanapata huduma hizo wanazungumziaje kampuni hizo ili mpate mwelekeo sahihi wa kazi zenu,” alisema.

Muliro alisema anaamini wamiliki wa kampuni ya SUKA wamefanya utafiti na kuamua kuingia kwenye utoaji wa huduma hiyo wakiwa na malengo makubwa ya kuboresha zaidi huduma hiyo kuhakikisha hakuna malalamiko ya wateja.

Kamanda Muliro alisema miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikilalamikiwa na wateja kwenye kampuni zilizokuwa zinatoa huduma kama hiyo ni tabia zisizo ridhisha za watu waliokuwa wakiendesha vyombo vya usafiri.

“Tabia zile zilishusha heshima ya huduma hiyo na watu walikuwa wakipata mrejesho wa lugha wanazopata kutoka kwa wahudumu wale , tabia ni pamoja na uvaaji ukihudumia watu lazima uvae mavazi ya heshima,” alisema

Aliwataka kutoa mafunzo ya mara kwa mara ya namna ya kutoa huduma hiyo ili kuhakikisha watoa huduma wanakuwa waadilifu kwa wateja na kuondoa malalamiko.

Naye Ofisa Mawasiliano wa SUKA, Luciana Mwambinga, alisema waliamua kuanzisha huduma hiyo baada ya kuona heka heka za maisha ya kila siku na mahitaji ya usafiri hasa kwa watu wasio na magari kwa kutengeneza daraja linalofanikisha mawasiliano kati ya watoa huduma na watumiaji kwa urahisi.

Alisema SUKA ni mfumo bora unaowaunganisha abiria na madereva kwa urahisi, ufanisi, usalama zaidi na kwa gharama nafuu ambapo wameboresha zoezi zima la upatikanaji wa usafiri kupitia mtandao kati ya abiria na watoa huduma ya usafiri.

“Tunatambua kuwa abiria na dereva wote wanahitaji mazingira bora yenye ufanisi na usalama ili waweze kufanya shughuli zao vyema na kwa kuzingatia hayo SUKA imelenga na inapatikana kwa watumiaji wote wa usafiri na tembelea www.sukaride.com

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!