MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Maftaha Nachuma amesema kuwa Serikali ya umoja wa Kitaifa (SUK)-imetokana na maridhiano ya chama chao (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo Chama cha ACT-Wazalendo hakijui misingi yake ndio maana kinakurupuka kutaka kujitoa. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).
Nachuma ameyasema hayo jana tarehe 14 Machi 2024, wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa SUK haikuundwa kukinufaisha chama cha siasa isipokuwa imeanzishwa kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar.
” “Hakuna chama kilichopitia magumu kama Chama cha Wanachi -CUF, sisi ndio chama ambacho watu wake wengi waliuawa mwaka 2001 hadi Rais mstaafu Hayati Benjamini Mkapa akaelezea kujutia kwa mauaji hayo ndio maana nasema hawa wanaojitoa SUK hawajui misingi ya SUK,” amesema Nachuma.
Amesema kuwa msingi wa kuundwa kwa serikali ya umoja unatokana na kuchoshwa na matukio ya umwagaji damu za wanachi na kuunganisha mawazo ya Wazanzibar wote kwenye serikali.
“Tunafahamu bado kuna matatizo ndani ya Serikali ya CCM lakini sio suala la kujitoa kwenye SUK kwa sababu rahisi rahisi tu” amesema Nachuma.
Nachuma, umeongea. Tunashangaa huyu ACT Makamu wa Rais, baada ya kwenda mbele anaturudisha kusiko.