Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mzee Mrema kuzikwa Alhamisi
Habari MchanganyikoTangulizi

Mzee Mrema kuzikwa Alhamisi

Spread the love

 

MWILI wa Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Agustino Lyatonga Mrema unatarajiwa kuzikwa Alhamisi tarehe 25 Agosti, 2022 nyumbani kwake Kiraracha- Marangu mkoani Kilimanjaro. Anaripoti Juliana Assenga, TUDARCo … (endelea).

Msemaji wa familia ya Mzee Mrema, Profesa Alex Mrema amewaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa mwili wa mwasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi, utaagwa katika Kanisa Katoliki Mbezi Salasala jijini Dar es Salaam kisha kusafirishwa kuelekea Marangu mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko.

Amesema chanzo cha kifo chake mwanasiasa huyo ni tatizo la mapafu.

Mrema alifariki jana asubuhi tarehe 21 Agosti, 2022 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa tangu tarehe 16 Agosti, 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

error: Content is protected !!