Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Simulizi baba wa binti aliyefariki Canada inasikitisha
Habari Mchanganyiko

Simulizi baba wa binti aliyefariki Canada inasikitisha

Spread the love

 

HATIMAYE Baba yake Hellen Kemunto, binti muuguzi raia wa Kenya aliyefariki wiki iliyopita nchini Canada, amejitokeza kuelezea maisha ya mwanaye.

Binti huyo alifariki wakati akiogelea ndani ya swimming pool tukio ambalo alikuwa akijirekodi live na kurusha kwenye mtandao wa Facebook kabla ya kuzidiwa na maji na kuzama. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Baba huyo anayefahamika kwa jina la John Nyabuto, amesema binti yake Hellen (24), alikuwa mtoto wa kwanza katika familia yake ya watoto sita na alikuwa tegemeo kubwa la familia.

Akizungumza na waandishi wa habari nchini Kenya jana tarehe 21 Agosti, 2022 amesema alihangaika kumsomesha mwanaye huyo hadi kidato cha nne na kushindwa kuwaendeleza ndugu zake Hellen watano kwa kuwa hakuwa na kipato kikubwa zaidi ya kilimo pekee.

“Hakuweza kuenda chuo kikuu. Alianza kufanya biashara ndogondogo hapa. Aliendelea hivyo mpaka huku akiwa na ndoto ya kuenda ng’ambo. Mimi niliona ni kama ndoto kwa sababu sina jamaa au rafiki yeyote wa kumsaidia kwenda huko,” Nyabuto alieleza gazeti la Nation.

Alisema baada ya muda binti huyo alibahatika kupata fursa ya kwenda kuishi na kufanya kazi nchini Canada kupitia mpango wa ‘Green Card’.

“Tatizo likawa nauli, kwa sababu siku na fedha… ilibidi nikope pamoja na fedha kidogo nilizokuwa nazo nikampatia akaelekea Canada kutimiza ndoto hiyo.

“Hellen alielekea huko mwaka 2018 na kuanza kufanya kazi na vilevile kuhudhuria masomo ya uuguzi.

“Sasa alikuwa anasoma stashahada ya uuguzi “Diploma in Nursing”, wakati hayuko shuleni alikuwa anaenda kibarua anapata hela kidogo anapata karo. Kidogo kilichokuwa kinabaki baada ya matumizi yake alikuwa anatukumbuka akawa ananitumia nikawa ninawalipia ada wadogo zake,” alisema.

Nyabuto alisema kuwa hatimaye Hellen aligeuka kuwa tegemeo lake kuu na wanawe wengine wakati alipoanza kulemewa.

Alisema hakuweza kuamini wakati alipopokea habari kuhusu kifo chake asubuhi ya Ijumaa.

“Nilikuwa naangalia WhatsApp nijue kama mtoto wangu alishinda vizuri. Hapo ndipo nilipata habari eti kuna habari mbaya kutoka kwa rafiki yake huko ng’ambo,”

Nyabuto alifichua kuwa aliona giza ghafla na kuangua kilio kikubwa baada ya kufahamishwa yaliyompata bintiye.

Wanafamilia wengine na majirani pia walijumuika naye kulia baada ya kuwaeleza habari hizo za kuhuzunisha.

Nyabuto alisema tayari amekubali kuwa amepoteza bintiye na kuomba msaada ili mwili wa marehemu uweze kuletwa Kenya kwa ajili ya mazishi.

‘Hata usiku sikulala, nilikuwa nawaza jinsi mwili utakavyofika hapa kwangu niuzike. Hiyo ndiyo shida ambayo niko nayo. Sijui gharama itakuwaje. Sijiwezi. Ndugu zangu pia hawajiwezi, kuna ndugu yangu ambaye pia aliaga,” alisema.

Hellen alifariki Alhamisi usiku, takriban dakika 10 wakati akijirekodi video kuirusha live Facebook akiwa kwenye swimming pool.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!