Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Lewandowski afungua akaunti ya mabao Barcelona
Michezo

Lewandowski afungua akaunti ya mabao Barcelona

Spread the love

 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Barcelona raia wa Poland, Robert Lewandowsik amefungua rasmi akaunti ya mabao katika klabu yake mpya baada ya jana tarehe 21 Agosti, 2022 kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao manne kwa moja dhidi ya Real Sociedad. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Mchezaji huyo aliyejiunga na miamba hiyo ya Hispania akitokea Ligi kuu ya Ujerumani katika klabu ya Bayern Munich, mechi hiyo inakuwa ni ya pili kuitumikia miamba hiyo baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa suluhu ya bila kufungana na Rayo Vallecano hivyo jana amefungua rasmi akaunti yake ya mabao.

Barcelona mpaka sasa wamecheza michezo miwili na kujikusanyia alama nne huku mashabiki wengi wa timu wakitarajia kupata matokeao mazuri kulingana na usajili wao walioufanya baada ya msimu uliopita kuisha bila kutwaa kikombe.

Mahasimu wao Real Madrid walitawala msimu huo kwa kubeba kombe la ligi kuu pamoja na Ligi ya mabigwa barani Ulaya

Aidha, mpaka sasa vita ya kuwania tuzo ya mfungaji bora inatazamiwa kuwa kali tangu mchezaji huyo ajiunge na Barcelona.

Lewandowsik anatarajia kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa mtaalamu wa kupachika mabao na mfungaji bora wa msimu uliopita Karim Benzema anaeitumikia klabu ya Real Madrid

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!