Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi ya bilioni 224 Singida
Habari Mchanganyiko

Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi ya bilioni 224 Singida

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amesema Mwenge wa Uhuru ambao umetoa mkoani humo kutokea Tabora, unatarajiwa kuzindua miradi yenye thamani ya Zaidi ya Sh 224 bilioni ambayo imetekelezwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Septemba  2023.

Miradi itahusu sekta ya elimu, afya, maji, nishati, kilimo, uchumi, miradi ya utunzaji wa mazingira na miundombinu. Anaripoti Danson Kaijage, Singida… (endelea).

Serukamba ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Septemba Iramba mkoani Singida wakati akipokea mwengehuo wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Balozi Batlida Briani.

Amesema lengo kubwa la kuupokea mwenge ni kufanya uchechemuzi wa miradi pamoja kuhamasisha upendo, amani na ushirikiano.

Akizungumzia sekta ya elimu amesema jumla ya Sh. 34.08 bilioni zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya elimu hususani ujenzi wa shule mpya za BOOST na shule mpya za sekondari kupitia mradi wa SEQUIP pamoja na utoaji wa elimu bila malipo kutoka shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Kwa upande wa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa,  Abdalla Shaib Kaim amesema lengo la kukagua miradi hiyo ni kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaendana na thamani ya fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!