Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Musoma Vijijini waomba shule za kidato cha tano, sita
Elimu

Musoma Vijijini waomba shule za kidato cha tano, sita

Spread the love

JIMBO la Musoma Vijjiini mkoani Mara, limeomba Serikali ianzishe shule za kidato cha tano na sita, huku likisema kuna baadhi ya shule zilizojengwa jimboni humo ziko tayari kupokea wanafunzi wa ngazi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara… (endelea).

Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, wakati ikitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa shule za sekondari unaofanywa na wananchi kwa kushirikiana na Serikali.

“Musoma Vijijini inaomba ipewe High Schools za masomo ya sayansi, sekondari sita zilizotajwa hapo juu ziko tayari kuanza kupokea Wanafunzi wa kidato cha tano na sita mwakani, Julai 2024,” imesema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, ofisi hiyo imeomba Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, kuwaunga mkono wananchi katika ujenzi wa shule hizo kwa kutumia mapato ya ndani.

“Halmashauri yetu (Musoma DC) inaendelea kushawishiwa na kuombwa nayo ianze kuchangia, kwa kutumia mapato yake ya ndani, ujenzi wa Maabara na Maktaba kwenye shule zetu,” imesema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wananchi kwa kushirikiana na Serikali pamoja na mbunge wao, wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa maabara za sayansi katika sekondari tano za kata, ikiwemo Sekondari za Mugango, Bugwema na Kiriba, huku Sekondari ya Makojo ikitarajiwa kukamilisha ujenzi huo mwishoni mwa Julai 2023.

Pia, ujenzi wa maabara za sayansi katika sekondari nyingine 19 unaendelea, ambao unatarajiwa kukamilisha kabla ya Julai 2023.

Hali kadhalika, wananchi wa jimbo hilo kwa kushirikiana na Serikali wanajenga shule nne mpya za sekondari, zikiwa na majengo ya maabara.

“Wananchi wanaishukuru Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Rais D.  Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu jimboni mwetu,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!