May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mrembo Mobetto atisha tena, apata dili nono

Hamisa Mobetto, mwanamitindo

Spread the love

 

MWANAMITINDO na msanii wa muziki wa bongo fleva Hamisa Mobetto, nyota yake imeendelea ku’ngaa baada ya kusaini mkataba mpya na kampuni ya kutengeneza nywele (Prima Afro). Anaripoti Matrida Peter…(endelea)

Mrembo huyo amesaini mkataba huo leo Agosti 16, jijini Dar es Salaam na kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo, katika miaka minne mfululizo.

Katika hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya Prima Afro Novatus Heshima amesema, kuwa “Tunayofuraha kufanya kazi na mrembo huyo kwa sababu ni kioo cha jamii pia ni mfano bora kwa warembo na watu wote wanaopenda kupendeza”

https://www.youtube.com/watch?v=7kkE5w3Tr6A

Pia amesema wataendelea kufanyanae kazi nyingine pia zaidi ya nywele kwani amekuwa ni mchapakazi  na kuzitangaza vyema bidhaa zao za nywele

Hata hiyo hamisa ametoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuendelea kumuamini ka kuahidi kufanya yale yote yaliyo ndani ya makubaliano yao.

Mrembo huyo amekuwa akilamba dili nyingi kipindi hiki na kufanya kazi na makampuni mbalimbali na hata serikalini, mara baada ya kuteuliwa kuwa moja ya wahamasishaji wa ulipaji kodi na waziri wa fedha na mipango mh. Mwigulu Nchemba.

error: Content is protected !!