Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa afanya ziara Dar, aipa rungu Takukuru
Habari Mchanganyiko

Majaliwa afanya ziara Dar, aipa rungu Takukuru

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na gharama za ujenzi wa miradi ya barabara ya Kijichi–Mwanamtoti yenye urefu wa kilomita 1.8 iliyogharimu Sh.5.4 bilioni na barabara ya Kijichi-Toangoma yenye urefu wa kilomita 3.25 iliyogharimu Sh.13.5 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu ameiagiza Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ihakikishe watu wote waliohusika na ubadhilifu huo wa fedha ambao tayari walishasimamishwa kazi wawe wamefikishwa mahakamani kabla ya tarehe 20 Agosti 2021.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 16 Agosti 2021, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara za Kijichi-Mwanamtoti na Kijichi-Toangoma wilayani Temeke na kituo cha Mabasi kilichopo Buza. Mirado hiyo inajengwa kupitia mradi uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP).

“Manispaa ya Temeke waliamua kutujengea mradi huu kwa kuongeza gharama kubwa za ujenzi. Tumeona namna mlivyoharibu fedha za nchi. Hatuwezi kujenga kilomita 1.8 ya lami kwa gharama ya shilingi bilioni 5.4 na hatuwezi kuwa na watumishi wa umma wa namna hii,” amesema.

“Watu wote waliohusika warudishwe na wafikishwe mahakamani, hatuwezi kufanya mchezo hizi ni fedha za walipakodi itakuwa ni mchezo kila mmoja anakuja anachukua fedha na kuondoka hatuwezi kujenga barabara ya kilomita 1.8 kwa gharama ya shilingi bilioni 5.4.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya ahakikishe anasimamia na anazingatia maslahi ya Wana-Temeke katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Wananchi Serikali yenu iko macho kweli kweli na hakuna sarafu itakayotoweka tunailinda na Mawaziri tupo kwa ajili hiyo na tuna maelekezo thabiti ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na watumishi wa umma tuko hapa kuwahudumia wananchi.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameiagiza Takukuru iwatafute viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke waliohusika katika kukopa shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ulipaji fidia ya ujenzi wa miradi mbalimbali warudishwe ili ajibu tuhuma zinazowakabili.

Mbali na agizo hilo, pia Waziri Mkuu ameelekeza kusimamishwa kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Buza hadi hapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu atakapojiridhisha ni mradi gani unapaswa kufanyika katika eneo hilo.

Pia, Waziri Mkuu ameiataka Takukuru ifanye uchunguzi ili kubaini ni kwanini uongozi wa Manispaa hiyo ulianza kulipa mkopo huo miezi miwili baada ya kuupokea mkopo huo huku mkataba ukionesha wanaweza kulipa deni hilo baada ya miezi sita kulingana na muda wa matazamio.

Akizungumzia kuhusu eneo la Temeke Kota, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na uongozi wa Manispaa ya Temeke wakutane na wafanye uamuzi juu ya matumizi ya eneo hilo na baada ya wiki moja wampelekee taarifa ya walichopanga kukifanya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!