June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ampongeza Rais mteule Zambia

Hakainde Hichilem

Spread the love

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais mteule wa Zambia, Hakainde Hichilem. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hichilem (59) ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) amemwanbusha Edger Lungu, aliyekuwa akitetea nafasi hiyo.

Mwanasisi huyo aliyegombea mara ya sita baada ya kushindwa kwenye awamu tano amepata kura 2,810,777 dhidi ya 1,814,201 alizopata Lungu.

Rais Samia amekuwa miongoni mwa waliomtumia salamu za rambirambi Hichilem.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Rais Samia amesema “kwa niaba ya Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali, nakupongeza Mhe. @HHichilema kwa ushindi ulioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia. Ushindi huo ni uthibitisho wa imani ya wananchi wa Zambia kwako. Naahidi kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu.”

error: Content is protected !!