Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mike Sonko apata pigo jingine, mahakama yasema alitolewa ofisini kwa haki
Kimataifa

Mike Sonko apata pigo jingine, mahakama yasema alitolewa ofisini kwa haki

Mike Sonko
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Juu nchini Kenya, imeamua kuwa Mike Sonko, aliyekuwa Gavana wa Nairobi, aliondolewa afisini kwa mujibu wa sharia, katiba na kanuni zilizowekwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Sonko aliondolewa madarakani, Desemba mwaka 2020, baada ya kukabiliwa na tuhuma lukuki, ikiwamo mashitaka ya  jinai kama utakatishaji fedha na ugaidi.

Mojawapo ya sifa kuu za mtu kutafuta kiti cha kuchaguliwa ni kwamba mgombeaji lazima awe hajapatikana na hatia ya kutumia vibaya ofisi ya serikali au ya umma au kukiuka Sura ya Sita ya Katiba.

Hata hivyo, mgombeaji anaweza kuruhusiwa kugombea ikiwa hajamaliza njia zote za kukata rufaa.

Katika kesi ya Sonko, amemaliza njia zote za rufaa, ikizingatiwa kesi yake ya kuondolewa mashitaka iliamuliwa na Mahakama ya Juu zaidi, Ijumaa iliyopita, 15 Julai.

Ni jukumu la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kutoa uamuziwa iwapo Sonko, ambaye aliyekuwa ameidhinishwa kugombea kiti cha ugavana katika kaunti ya Mombasa Alhamisi, 14 Julai, atagombea au la.

Iwapo tume ya uchaguzi itakubali ugombeaji wa Sonko, mwanya huo unaweza kupingwa mahakamani, ikizingatiwa kuwa Sonko sasa amemaliza chaguzi zake zote za rufaa.

Sonko alikuwa ameidhinishwa na Mahakama Kuu ya Mombasa kuwania wadhifa huo. Anataka kumrithi Ali Hassan Joho, kama gavana wa pili wa eneo la Mombasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!