August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Stars yaingia kambini hii leo

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kikiwa mazoezini

Spread the love

 

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzani (Taifa Stars) kimeingia kambini hii leo tarehe 15 Julai, kujiandaa na mchezo wa kufuzu kwa michuano ya kombe la Mtaifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Taifa Stars ambayo ipo chini ya kocha mkuu Kim Poulsen imeingia kambini kwenye Hotel ya Tiffan, jijini Dar es Salaam na siku ya kesho kuanza maandaliz ya michezo hiyo miwili.

Katika kampeni hiyo ya kutafuta tiketi ya kufuzu, Stars itamenyana dhidi ya Somalia huku michezo hiyo yote miwili ikipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza utakuwa utakuwa tarehe 23 Julai 2022, ambapo Somalia watahesanika kama wanyeji, licha ya kutumia uwanja wa mkapa na mchezo wa marudiano utakuwa tarehe 30 Julai 2022.

Kama Stars itafanikiwa kuvuka hatua hiyo, itamenyana na Uganda kwenye mchezo wa mzunguko wa pili na kama wakifanikiwa kuwaondoa waganda, basi timu hiyo itafuzu kwa mara ya tatu kwenye michuano hiyo.

Michuano hiyo inatarajia kuchezwa mwakani 2023, katika nchini ya Algeria kuanzia Januari 6 mpaka 30, 2023.

error: Content is protected !!