Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Mgogoro wa ardhi wakwamisha ujenzi nyumba ya walimu Ileje
Elimu

Mgogoro wa ardhi wakwamisha ujenzi nyumba ya walimu Ileje

Spread the love

MGOGORO wa mpaka kati ya vijiji vya Sange na Mswima kata ya Sange wilayani Ileje mkoani Songwe umetajwa kukwamisha ujenzi wa nyumba ya walimu yenye thamani ya Sh 100 milioni. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe …(endelea).

Kusimama kwa ujenzi huo kulitokana na wananchi wa Kijiji cha Mswima kudai eneo inapojengwa nyumba hiyo ni eneo la Kijiji chao huku wananchi wa Kijiji cha Sange wakidai ni eneo halali la shule tangu ilipoanza.

Kitendo cha kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro huo kimesababisa mradi huo kusimama licha ya fedha Sh mbili milioni kutumika kujenga msingi.

Kutokana na mzozo huo jana tarehe 17 Julai 2023 Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo kupitia kwa Mwenyekiti wake, Patrick Ghambi walipotembelea eneo hilo waliagiza nyumba hiyo ijengwe kwa kuwa ni eneo halali la shule na limeshapimwa.

Ghambi alisema maamuzi ya kuhamishwa eneo ambalo awali palijengwa msingi yatakuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Alisema hakuna sababu za msingi kwa wananchi wa vijiji hivyo kugombea eneo la shule.

“Nawashangaa sana wananchi wa Mswima ambao ndio waanzilishi wa mgogoro huu. Ni eneno ambalo wananchi wengi wamesoma shule ya msingi Sange na wanajua mipaka ya shule…kwanini mlete migogoro ambayo haina tija?” alihoji Ghambi.

Ghambi alisema viongozi kuanzia ngazi ya vijiji mpaka wilaya wahakikishen wanaweka alama za mipaka ya taasisi ili kuepusha migogoro ambayo imezuia kuendelea kwa ujenzi wa nyumba ya walimu.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Ileje na mjumbe wa kamati ya siasa, Ubatizo Songa alisema wilaya walitenga zaidi ya sH 20 milioni  kwa ajili ya kupima maeneo yote ya taasisi ikiwepo na shule ya msingi Sange.

Alisema eneo hilo lipo kisheria kwani elimu haina mpaka hivyo ujenzi uendelee kama kawaida watakaoendelea kukwamisha watawajibishwa.

Mwenyekiti wa shule ya msingi Sange, Zawadi Kabuje alisema mgogoro huo unahusishwa na mvutano wa kisiasa hali ambayo imechelewesha mradi ambao ulipaswa kukamilika tangu tarehe 30 Juni mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!