Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara SBL yaja na kampeni ya ‘Jibambe Kibabe’
Biashara

SBL yaja na kampeni ya ‘Jibambe Kibabe’

Irene Mutiganzi, Mkuu wa Masoko ya Vinywaji Vikali, Serengeti Breweries Limted
Spread the love

 

KAMPUNI ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua kampeni yake kubwa ya kitaifa ‘Jibambe Kibabe’ inayolenga kuchochea uwezeshaji kiuchumi katika mfumo wake mzima wa biashara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Chini ya kampeni hiyo iliyozinduliwa rasmi leo Jumanne, Julai 18, 2023, SBL itatoa motisha kubwa, marejesho ya fedha, na punguzo kwa washirika wake wa biashara wanaponunua bia na vileo vya SBL.

Washindi wa kampeni ya ‘Jibambe Kibabe’ kutoka mtandao wa biashara wa SBL ni pamoja na wauzaji wakubwa, wauzaji jumla, wasambazaji na maduka ya rejareja.

Irene Mutiganzi, Mkuu wa idara ya Vileo wa SBL, amesema kampeni ya ‘Jibambe Kibabe’ ilianzishwa lengo la kuwawezesha washirika wa kibiashara wa SBL, haswa katika mazingira ya uchumi ya sasa ambapo biashara zinakaribia kupona kutokana na kutokuwa na uhakika wa kiuchumi.

Mutiganzi alielezea kuwa katika miaka iliyopita, kama ilivyo kwa biashara nyingine nyingi, SBL na washirika wake wa biashara wamekabiliana na changamoto kutokana na mazingira ya kiuchumi ya kimataifa yanayojitokeza.

Akiitambua changamoto hizo zinazoshirikishwa, alielezea jinsi SBL inavyojivunia maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa kutokana na uvumilivu mkubwa ambao kampuni yake na washirika wake wameendelea kuonyesha.

Akifafanua kuhusu muundo wa kampeni hiyo, Mutiganzi alisisitiza kuwa kampeni hii inawapatia wateja wanaofanya vizuri punguzo na marejesho ya fedha, na pia kuwapa fursa ya kupata soko kutokana na athari inayotarajiwa ya kampeni hiyo inayosukuma ununuzi zaidi.

“Pia kampeni hii pia inajumuisha kipengele kinachowazawadia wafanyakazi wa baa (wahudumu) kwa kila chupa wanayouza kwa kufikia malengo yao.

“Wengine wanaonufaika na ‘Jibambe Kibabe’ ni watumiaji katika kiwango cha baa ambapo kampeni hiyo imeandaa ofa za kubebea (bucket deals) zilizo tengenezwa maalum kwa watumiaji kufurahia na kushiriki na marafiki kwa bei iliyopunguzwa, hatimaye kutoa akiba kwa wote,” alisema Mutigazi.

Nicholas Chonya, Meneja Mauzo wa Kanda wa Serengeti Breweries Limted akifafanua jambo juu ya kampeni ‘Jibambe Kibabe’

Naye, Nicholas Chonya, Meneja Mauzo wa Serengeti Kanda ya Dar es Salaam amesema kampeni hiyo itahusisha vinywaji vyetu vyote, kwa maana ya bia na baadhi ya pombe kali zinazotengenezwa na kampuni ya bia ya Serengeti.

“Nitoe wito na msisitizo kwa washirika wetu wa kibiashara, kuanzia wasambazaji mpaka mlaji wa mwisho, kushiriki kwa wingi,” alisema Chonya na kuongeza.

“Kwa mfano kupitia kampeni hii, wauzaji wa baa wanaofikia asilimia 50%  ya malengo yao ya mauzo watajipatia kiasi cha fedha kuanzia shilingi 100 kwa chupa moja ya bia, mpaka Sh. 1,000 kwa chupa moja ya pombe kali.”

Jonas Sindabaha, Msambazi wa vinjwaji vya Kampuni ya Serengeti, akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Jibambe Kibabe’

Kwa upande wake mwakilishi wa wasambazi wa vinywaji vya Serengeti, Jonas Sindabaha, alisema anawapongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuandaa kampeni hii ya ‘Jibambe Kibabe’ ambayo imelenga kuwanufaisha wanaofanya nao biashara kwa ukaribu.

“Hii inatudhihirishia kuwa Serengeti ni washirika wetu wa kibiashara wa kweli, wanaojali maslahi yetu. Hivyo niwapongeze kwa hatua hii,” alisema Sindabaha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!