Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakili Madeleka kusota rumande hadi Julai 31, sababu zatajwa
Habari MchanganyikoTangulizi

Wakili Madeleka kusota rumande hadi Julai 31, sababu zatajwa

Peter Madeleka, Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Spread the love

 

IMEBAINIKA kuwa sababu ya Wakili Peter Madeleka, kukamatwa tena jana Jumatatu na Jeshi la Polisi ni kufufua kesi ya uhujumu uchumi Na./2020 iliyokuwa inamkabili baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuifuta. Anaripoti Mariam Mdhihiri, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 18 Julai 2023 na Wakili Simon Mbwambo, ambaye anamtetea Wakili Mdeleka, akizungumza na MwanaHALISI Online, juu ya sababu za mteja wake kukamatwa muda mfupi baada ya mahakama hiyo mbele ya Jaji Aisha Bade, kutoa uamuzi huo jana asubuhi.

Jaji Bade alitoa uamuzi wa kufuta makubaliano ya kisheria ya kukiri kosa na kulipa fidia “Plea bargaining”, kupitia maombi Na. 80/2021, yaliyowasilisha na Wakili Madeleka, kupinga makubaliano hayo yaliyotokana na kesi ya uhujumu uchumi Na. 40/2020, akidai yalikuwa kinyume cha sheria.

Baada ya kufuta makubaliano hayo yaliyoingiwa na Wakili Madeleka, pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Jaji Bade, alitoa uamuzi wa kesi ya msingi kuendelea pale ilipoishia kabla ya kufikia Plea Bargaing.

“Madeleka aliingia mkataba wa kukiri kosa na kulipa fidia katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili, 2021 baada ya kuingia makubaliano hakuridhika na hivyo akakata rufaa mahakama kuu.

Uamuzi umetolewa kwamba shauri lirudishwe sababu mwenendo mzima wa Plea Bargaining umeendeshwa vibaya, hivyo imeamuru shauri lirudi liendelee kabla mkataba huo kuingiwa,” amedai Wakili Mbwambo.

Wakili huyo amedai “jana amekamatwa na kupandishwa kizimbani kwa kurudishiwa shauri lake la awali la uhujumu uchumi, kutokana na maamuzi ya Mahakama Kuu ya leo.”

Wakili Mbwambo amedai mteja wake bado yuko katika mahabusu ya Gereza la Kisongo, jijini Arusha, licha ya kujenga hoja kwamba Wakili Madeleka aachiwe kwa dhamana, kwani wamefungua maombi ya kwenda Mahakama ya Rufani, hivyo kesi ya msingi isubiri maamuzi ya rufani.

Lakini Jaji Bade alisema hawezi kutoa uamuzi huo hadi atakapopata nyaraka zinazothibitisha ufunguaji wa maombi hayo.

Wakili Mbwambo amedai, Wakili Madeleka atasota rumande hadi tarehe 31 Julai mwaka huu, wakati kesi hiyo itakapokwenda kusikilizwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!