Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara DC Momba ajitosa mkataba bandari, aeleza Tunduma itakavyofaidika
Biashara

DC Momba ajitosa mkataba bandari, aeleza Tunduma itakavyofaidika

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Faki Lulandala amejitosa katika sakata la mjadala kuhusu mkataba wa uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam na kuwataka Watanzania kupuuza upotoshaji unaotolewa na baadhi ya watu wasiokuwa na uzalendo. Anaripoti Ibrahim Yassin…(endelea).

Amesisitiza kuwa uwekezaji katika bandari hiyo ya Dar es Salaam utaziongezea faida wilaya za mkoa wa Songwe hususani Mji wa Tunduma ambao ndio lango la nchi za Kusini mwa Afrika kwa kuongeza wigo wa mapato kutokana na mizigo itakayoongeza katika upakuaji kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana tarehe 17 Julai 2023, amesema zaidi ya asilimia 65 ya mizigo ambayo hushushwa katika Bandari ya Dar es Salaam hupita katika mpaka wa Tunduma kuelekea nchi za kusini mwa Afrika.

“Kupitia chanzo kimoja cha mapato cha magari makubwa yanayotoka bandarini kupitia mpaka wetu wa Tunduma tunakusanya Sh nane milioni mpaka 10 milioni kwa siku, Hivyo maboresho na uwekezaji wa DP World katika bandari yetu yatatusaidia kuongeza ukusanyaji wa mapato katika Mji wetu wa Tunduma,” alisema.

Alisema faida nyingine watakayoipata ni pamoja na kujenga bandari kavu katika mji wa Tunduma ambapo tayari walishatenga ekari 2000 kwa ajili ya uwekezaji huo.

“Tunawakaribisha wawekezaji wenye uwezo kuja kuwekeza katika eneo letu wawe wa ndani ya nchi yetu au kutoka nje bila kujali rangi, hata DP World tunawakaribisha kuwekeza Tunduma kujenga bandari kavu,” alisema.

Alisema Momba ni wanufaika wakubwa wa bandari ya Dar es Salaam, kupitia mapato ya ndani Halmashauri ya mji Tunduma imefanikiwa kuajiri watumishi 52 ambao wanalipwa kupitia mapato ya ndani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!