Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Dk. Mwinyi atangaza mapumziko mwaka mpya wa kiislamu
Habari za Siasa

Rais Dk. Mwinyi atangaza mapumziko mwaka mpya wa kiislamu

Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi ametangaza siku kuu ya mwaka mpya wa dini ya kiislamu, kuwa mapumziko visiwani humo. Anaripoti Maryam Mdhihiri, Dar es Salaa…(endelea).

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, ametangaza mapumziko hayo kupitia tamko lake lililochapishwa katika Gazeti la Serikali, tarehe 14 Julai 2023.

Kwa mujibu wa tamko hilo, Rais Mwinyi ametangaza mapumziko kupitia mamlaka ya kikatiba aliyopewa chini ya kifungu cha 6(1)(a), cha Sheria ya Masuala ya Rais wa Zanzibar, Namba 3 ya 2020.

Kufuatia tangazo hilo, siku ya Jumatano, tarehe 19 Julai 2023, ambayo itaangukia mwaka mpya wa kiislamu, itakuwa mapumziko visiwani Zanzibar.

“Siku hii huadhimishwa kila mwaka kwa kumbukumbu ya Hijra, ambayo ni safari ya Mtume Muhammad (S.A.W). Hijra hii ilikuwa hatua muhimu katika historia ya uislamu, kwa kuanzishwa utawala wa kiislamu Madina. Mabadiliko hayo ya kihistoria yaliunganisha wasilamu katika kutekeleza imani na kujenga jamii yenye misingi ya kidini,” limesema tamko la Rais Mwinyi.

Uamuzi huo wa Rais Mwinyi, unakuja siku chache baada ya Ofisi ya Mufti Zanzibar, kuomba siku kuu ya mwaka mpya wa kiislamu kuwa mapumziko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!