Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania, Hungary wafungua mazungumzo uwekezaji na biashara
Habari za Siasa

Tanzania, Hungary wafungua mazungumzo uwekezaji na biashara

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania na Hungary, zimefungua majadiliano kuhusu uimarishaji mahusiano ya kidiplomasia katika masula ya uwekezaji na biashara. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 18 Julai 2023 na Rais Samia Suluhu Hassan, akielezea mazungumzo aliyofanya Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Hungary, Katalin Novak, aliyeko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne iliyoanza jana Jumatatu hadi tarehe 20 Julai mwaka huu.

“Wakati wa mazungumzo yetu ya pande mbili, tulipata nafasi ya kujadili masuala mapana yenye maslahi kwa mataifa yetu mawili na watu wetu. Tumeainisha maeneo ya kimkakati na namna ya kuimarisha ushirikiano wetu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ametaja maeneo ya ushirikiano ambayo Tanzania na Hungary, watashirikiana, ikiwemo uimarishaji baishara na uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo, nishati mbadala,  utalii, madini, uvuvi, viwanda, fedha na elimu.

“Katika biashara na uwekezaji, tumetambua kwamba biashara na uwekezaji kati yetu imekuwa chini, ambapo 2022 ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani 4.2 milioni. Lakini kuna namna ya kuimarisha na kupanua,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema amekubaliana na Rais Novak, kuimarisha masuala ya uwezeshaji wanawake.

“Katika elimu, Hungary imekuwa mshirika muhimu kwa Tanzania hususan katika elimu ya juu. Kwa pamoja tumeamua kuendeleza ushirikiano wetu. Wanafunzi kutoka Hungary watakuja Tanzania kusoma katika vyuo vyetu na katika hili tutaanza na watano wakati Hungary watachukua wanafunzi wetu 30,” amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Rais Novak, amesema lengo la Hungary ni kuwa na ushirikiano na Tanzania, bila kuingilia mambo yake ya ndani.

“Niko hapa nawakilisha nchi ya Hungary, nchi yetu siyo kubwa lakini ni taifa linaloheshimika na tumekuja Tanzania tunataka kuwajua na kuwaelewa maisha yenu halisi. Hatutaki kuingilia siasa zenu za ndani na maamuzi ya ndani na tunafurahi kwamba na nyie ni taifa linaloheshimika,” amesema Rais Novak.

Aidha, Rais Novak, amesema amefurahi kufanya mazungumzo na Rais Samia ambaye jinsia zao zinafanana, kitendo kinachowapa jukumu la kusaidia kuwainua wasichana na wanawake kutimiza ndoto zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!