Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Maadhimisho wiki ya msaada kisheria yazinduliwa, mambo manne kutikisa
Habari Mchanganyiko

Maadhimisho wiki ya msaada kisheria yazinduliwa, mambo manne kutikisa

Spread the love

MAADHIMISHO ya wiki ya msaada wa kisheria Zanziba kwa 2023, yamezinduliwa huku masuala matano yakitarajiwa kufanyika kwenye zoezi hilo, ikiwemo utoaji elimu na makundi yaliyoko vizuizini kutembelewa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Serikali ya Zanzibar, kupitia Idara yake ya msaada wa kisheria, kwa kushirikiana na Legal Service Facility (LSF), yamezinduliwa leo tarehe 15 Julai 2023 na Waziri wa Ofisi ya Rais. Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman.

Akizungumza wakati wa akizindua maadhimisho hayo, Suleiman amesema yameandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha Zanzibar inazungukwa na jamii yenye ustawi mzuri kisheria.

“Shughuli hii ni muhimu kwa kuwa tunalenga kuhakikisha kuwa, Zanzibar inazungukwa na jamii yenye ustawi mzuri uliomarika katika kila nyanja ya maisha, pamoja na kuhakikisha wananchi wake hususani wanyonge na wasiojiweza wanapatiwa msaada wa kisheria bila ya usumbufu wowote. Lengo kuu la wiki ya msaada wa kisheria ni kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa jamii yetu inayotuzunguka,” alisema Suleiman.

Naye Afisa Programu Mwandamizi wa LSF Zanzibar, Alphonce Gura, alisema shirika lake limeshiri kuandaa maadhimisho hayo ili kuendeleza juhudi zake za kukuza upatikanaji haki, kupitia uwezeshaji wa kisheria kwa wananchi wote.

“LSF kazi yetu kubwa ni kukuza upatikanaji wa haki kupitia uwezeshaji wa kisheria kwa wananchi wote hususani wanawake na wasichana. Hivyo kupitia maadhimisho haya tutaweza kuwafikia watu wote kupitia shughuli mbalimbali ambazo zinakwenda kufanyika katika kipindi hiki cha maadhimisho,” alisema Gura.

Matukio mengine yatakayotekelezwa katika maadhimisho hayo, ni utoaji elimu ya kisheria, uendeshaji jukwaa la kona ya msaada wa kisheria ili kuyafikia makundi yote katika jamii, kutembelea makundi yaliyoko vizuzini, kama magereza, rumande na vyuo vya mafunzo.

Pamoja na uandaaji bonaza la msaada wa kisheria kwa ajili ya kupaza sauti kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji katika jamii.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, tarehe 22 Julai mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!