WAMILIKI wa meli kutoka Estonia wamesema meli yao imezama katika pwani ya Ukreini baada ya kutokea mlipuko. Inaripoti BBC … (endelea).
Wamiliki hao wamesema watumishi wawili wa meli hiyo waliokolewa na wengine wanne walipotea kwa muda na baadaye wote kuokolewa na timu ya uokozi ya Ukreini.
Meli hiyo inayopeperusha bendera ya Panama inamilikiwa na kampuni ya Vista yenye makao yake Estonia ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Kujihami NATO na inapakana na Urusi.
Meli hiyo iliingia Pwani ya Ukreini baada ya siku chache zilizopita kuondoka katika bandari ya Chornomorsk karibu na Odesa. Hata hivyo bado haijajulikana sababu ya mlipuko huo.
Jeshi la Ukreini limesema Urusi imekuwa ikituma manuari kwa lengo la kuiteka Odesa, jiji la watu zaidi ya milioni moja na lenye bandari muhimu.
Leave a comment