Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kuachiwa Mbowe: Shangwe zaibuka mahakamani, Kibatala afunguka
Habari za SiasaTangulizi

Kuachiwa Mbowe: Shangwe zaibuka mahakamani, Kibatala afunguka

Spread the love

 

SHANGWE zimeibuka katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam, baada ya mahakama hiyo kufuta kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tukio hilo limetokea leo Ijumaa, tarehe 4 Machi 2022, muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, kuwasilisha hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu ya kutokuwa na nia ya kuendlea na kesi hiyo.

Mbali na Mbowe, wengine waliokuwa wanashtakiwa katika kesi hiyo iliyokuwa na mashtaka ya ugaidi matano, ni Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Baada ya Jaji Tiganga kutoa amri ya kesi hiyo kufutwa na kuagiza Mbowe na wenzake watolewe magereza leo hii, mawakili wa utetezi na wanachama wa Chadema walioko mahakamani hapo walianza kuimba na kushangilia.

Mawakili wa Utetezi, akiwemo Peter Kibatala na Dickson Matata, walikuwa wanaimba nyimbo iliyosema “niko tayari kulipa gharama sitasimama maovu yakitawala.”

https://www.youtube.com/watch?v=6OLXZcQ_zJ4

Baaada ya Jaji Tiganga kuondoka mahakamani hapo, Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Wakili Kibatala, alizungumza na wanahabri kuhusu hatua hiyo, akisema wamefurahi baada ya DPP Mwakitalu kuamua kuondoa mashtaka.

“Kwanza tunafurahi sababu wateja wetu ambao wamekaa muda mrefu, ukitoa Mbowe ambaye amekaa miezi tisa gerezani, lakini wale vijana ambao wameitumikia nchi yao kwa jasho na damu kwenye mazingira ambayo dunia imesikia wamewekwa gerezani,” amesema Wakili Kibatala.

Kibatala amesema, mawakili wa utetezi katika kesi hiyo walitoa jasho na damu lao mahakamani hapo, kuhakikisha Mbowe na wenzake wanaachwa huru.

“Mimi binafsi nianze kwa kushukuru jopo la mawakili ambao pamoja nami walipigana kiume na kike kwa kutegemea jinsia zao,” amesema.

“Tanzania na dunia nzima imeshuhudia hakuna kitu chochote tumekiacha, tumetoa jasho, damu na mioyo yetu tumeiacha mahakamani. Ninasikia fahari mawakili wenzangu ambao walikuwa hawafahamiki wao nani wanafahamika na kazi zao zinajukikana,” amesema Wakili Kibatala.

“Safari ilikuwa ndefu, nilisimamia kesi tatu za ugaidi watu wakaachiwa huru, lakini hii impact yake ilikuwa kubwa. Cha msingi tulijitahidi kutumia ujuzi wetu wote hata pale palipokuwa na mabonde tulijua safari yetu itaishia wapi,” amesema Wakili Kibatala na kuongeza:

“Ni safari ndefu sio kazi rahisi, nimesimamia hii kesi ya Mbowe ambayo inatazamwa nchini na duniani kote. Presha zilikuwa kubwa tuko very proud tuliacha kila kitu chetu mahakamani, dunia na nchi mliiona hilo,” amesema

Aidha, Kibatala amempongeza kwa dhati, Askofu wa Kanisa la Uamusho la Morovian, Emmaus Mwamakula kwa jinsi alivyojitoa wakati wote na kufika mahakamani na wakati mwingine alikuwa akiwaombea pale walipokuwa wakihisi kutetereka.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

TAMISEMI yatenga bil. 17.79 kwa ajili uchaguzi serikali za mitaa

Spread the loveWIZARA Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imetenga fedha kiasi cha Sh. 17.79...

Habari za Siasa

CAG abaini madudu katika vyama 10 vya upinzani

Spread the loveUKAGUZI wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!