Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Kubenea kuhojiwa Polisi Dar 
Habari za Siasa

Mbunge Kubenea kuhojiwa Polisi Dar 

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Saed Kubenea  amemtaka mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini Profesa Ibrahim Lipumba kuacha kulipotezea muda Jeshi la Polisi na kwamba aliache lifanye kazi yake , anaandika, Irene David.

Kauli hiyo ya Kubenea ikiwa ni siku moja baada ya Profea Lipumba kukimbilia Polisi Kanda maalum ya  Dar es salaam, akilalamika kwamba anatishiwa na mwanasiasa kutolewa katika ofisi yake iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.

Wasiwasi huo umeibuka mara baada ya Uongozi wa Kanda ya Pwani na Dar es salaam (Chadema)  na viongozi wa CUF wanaomuuunga mkono Maalim Seif  wakiongozwa na Kubenea, wiki iliyopita kuanzisha operesheni ya Ondoa Msaliti Buguruni(OMB), kwa lengo la kumng’oa Profesa Lipumba ambaye ni msaliti.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kubenea amesema amepokea wito wa polisi kwa njia ya simu na kwamba kesho mchana ataripoti polisi, lakini pia ameongeza kuwa kwa namna yoyote  ile hatayumbishwa mpaka ahakikishe wanamng’oa ofisini msaliti huyo.

“Bado adhima ya kumwondoa msaliti Buguruni ipo palepale na haiwezi kurejeshwa nyuma kwa maneno rejareja na ahadi za uongo ama vitisho vya aina yoyote,”

“Lipumba ni msaliti ni lazima aondoke na katika hili ntauza hata kiatu changu lakini ataondoka.” amesema Kubenea.

Pomoja na hayo kubenea amesema, tayari matawi ya Chechinia, Hosigofina, Palestine, Kosovo, Saratoga, Arafati yote yameonyesha nia ya kumuunga mkono

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!