Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu azua kizazaa mahakamani Dodoma
Habari za Siasa

Lissu azua kizazaa mahakamani Dodoma

Kulia: Tundu Lissu akiondoka mahakamani baada ya kuhakikishia na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa (picha ya kushoto).
Spread the love

MWANASHERIA wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu leo ametumia zaidi ya saa nne akiwa katika mahakama ya wilaya Dodoma akigoma kutoka humo akihofia kukamatwa, anaandika Dany Tibason.

Lissu akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma amesema jana majira ya asubuhi mke wake alimpigia simu na kumueleza kuwa askari kanzu wapatao sita walifika nyumbani kwake Dar es salaam wakimtafuta.

Hata hivyo, Lissu amesema akiwa mjini Dodoma akiendelea na kesi ya walimu ambao ni wateja wake alipokea taarifa kuwa wapo askari nje ya mahakama wanamsubiri wamkamate.

Kutokana na taarifa hiyo Lissu aligoma kutoka mahakamani hapo hatua ambayo ilisababisha kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa kwenda kumuona na kumhakikisha kwamba hakuna mtu anayemtafuta.

Kauli hiyo ya Mambosasa ilimpa uhakika Lissu na hivyo kuamua kutoka nje ya Mahakama na kuendelea na shughuli zake.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!