Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mapatano ya kibinadamu yatangazwa Ethiopia
Kimataifa

Mapatano ya kibinadamu yatangazwa Ethiopia

Spread the love

 

SERIKALI nchini Ethiopia imetangaza maafikiano ya kibinadamu , katika mzozo wake uliodumu takribani miezi 16 na Wanajeshi kutoka eneo la Kaskazini mwa Tigray. Inaripoti BBC … (endelea).

Vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe, vimeacha zaidi ya watu milioni tano wakiwa na uhitaji wa msaada wa chakula, hakuna chochote kilichofikishwa Tigray tangu katikati ya Desemba.

Taarifa hiyo inakuja baada ya ziara ya Ethiopia ya Mjumbe Maalumu wa Marekani David Satterfield kusema kwamba vikosi vya Tigrayan bado havijajibu hatua hiyo ya Serikali.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), anayefahamika kwa jina la Tedros Adhanom Ghebreyesus ,anayetoka Tigray, ameelezea hali ya huko sio nzuri na kuishutumu Serikaki ya Ethiopia kuzuia kupeleka msaada huko.

Hata hivyo Serikali inakishutumu Chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kwa kuzuia wasambazaji wa misaada.

Katika taarifa ya siku ya alhamisi tarehe 24 machi 2022 , Serikali ilisema kuwa mapatano hayo ni ya muda usiojulikana yanafaa yaanze mara moja kwakuwa yataboresha Maisha ya watu wa Kasikazini mwa nchi ikiwa tu hatua hiyo itachukuliwa.

Aidha mapigano hayo alianza Novemba mwaka 2020, kufuatia miezi kadhaa ya mvutano kati ya mamlaka ya shirikisho ya TPLF ,ambayo ilitawala Tigray.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!