MAHAKAMA ya Haki ya Afrika Mashariki leo Ijumaa tarehe 25 Machi 2022 itatoa hukumu ya kesi juu ya uhalali wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).
Kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2020, ilifunguliwa na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake wakipinga mabadiliko ya sheria hiyo.
Mbowe na wenzake wanalalamikia ukiukwaji wa Mkataba wa Afrika Mashariki wa masharti ya utawala bora na haki za binadamu ambapo mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa yam waka 2019 inaonekana kukiukwa.
Miongoni mwa vifungu vinavyobishaniwa kwenye sheria hiyo ni pamoja na cha 5A(1) kinachozuia mtu au taasisi kutoa elimu ya uraia bila idhini ya msajili wa vyama vya siasa.
Aidha, Mbowe na wenzake wanalalamikia kifungu cha 5B(1) kinachotoa mamlaka kwa msajili kuhitaji taarifa yoyote ya chama, vifungu 6B(d),8C(2),8D(2),8E,11A(2),21(E) na 23(7).
Mbowe na wenzake wanawakilishwa na mawakili John Mallya na Jebla Kambole ambapo tayari Mbowe na Mallya wamekwisha kufika mahakamani hapo.
Leave a comment