KIONGOZI nchini Afrika Kusini wa kundi linalopinga wahamiaji, amekamatwa siku ya Alhamisi tarehe 24 machi 2022 vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti.
Nhlanhla Lux Dlamini mwenye umri wa miaka 33 ,ameripotiwa kuzuiliwa katika kituo cha Polisi katika mji mkuu wa kibiashara wa Johannesburg.
Hata hivyo sababu za kukamatwa kwake bado hazijabainika.
Kundi lake linalofahamika kwa jina la Operation Dudula ,limekuwa likifanya kampeni dhidi ya Raia wa kigeni wasio na vibali nchini.
Aidha uungwaji mkono wa kundi hilo, umekuwa ukiongezeka miongoni mwa jamii ya Waafrika Kusini wanaohisi kutengwa.
Kuna wasiwasi kwamba kampeni zake ,zinaweza kusababisha kuzuka kwa ghasia za chuki dhidi ya wageni nchini
Leave a comment