SHIRIKA la Afya Duniani limetoa wito wa tahadhari , juu ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya nchi za Kiafrika zinazolegeza uchunguzi wa Covid 19, na hatua za kukabiliana na virusi hivyo. Inaripoti BBC … (endelea).
WHO inasema kwamba “janga hili ni la kutisha , katika bara ambalo linaviwango vya chini Zzaidi vya chanjo Ulimwenguni.”
Hata hivyo lilisema kuwa kwasababu ya shinikizo la kufungua Uchumi ,nchi zinazopunguza ufuatiliaji na hatua nyingine.
“Ni jambo la kutia wasiwasi kwamba karibu nusi ya nchi zote barani Afrika, zimeacha kufuatilia mawasiliano ya visa hii ni pamoja na upimaji wa virusi ndio uti wa mgongo wa mwitikio wote wa janga,” alisema Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika ya WHO , katika mkutano wa waandishi wa habari Alhamisi tarehe 24 Machi 2022.
Taadhari hiyo ya WHO inakuja huku kukiwa na ongezeko la hivi majuzi ,la visa vya Covid 19 katika sehemu nyingi Ulimwenguni.
“Kuondoa vikwazo vya Kiafya kwa Umma, haimaanishi kuinua mguu kutoka kwa tahadhari ya janga hilo,” DK Moeti amesema.
Takribani Watu milioni 201 au 15% ya watu , wa Afrika wamepatiwa chanjo kamili ikilinganishwa na wastani wa Kimataifa wa 57% kulingana na Shirika hilo
Leave a comment