Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Makamanda 6 Hamasa wadaiwa kuuawa
Kimataifa

Makamanda 6 Hamasa wadaiwa kuuawa

Spread the love

Jeshi la Israel linadai kuwa hadi sasa limeshawaua viongozi sita wa juu wa kundi la Hamas tangu kuanza vita dhidi ya Ukanda wa Gaza kufuatia uvamizi wa kundi hilo lilioua na kuwateka nyara wanajeshi na raia kadhaa wa Israel. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Jeshi la Israel (IDF), viongozi hao wenye vyeo vya juu waliouawa ni pamoja na maafisa wa kisiasa na kijeshi.

Taarifa ya IDF imewataja pia viongozi wawili wa Hamas ambao waliuawa wiki iliyopita, akiwemo Waziri wa Uchumi wa Hamas, Jawad Abu Shamala, na Zakaria Abu Maamar, ambaye inasemekana alihusika na masuala ya mahusiano ya kimataifa.

Jana Jumapili, Israel iliendeleza usiku kucha mashambulizi dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa lengo la kulisambaratisha kundi la Hamas, lakini viongozi wengi wa kundi hilo linalozingatiwa na Umoja wa Ulaya na Marekani kama la kigaidi, wanaishi nje ya nchi.

Juhudi za kidiplomasia zimekuwa zikiongezeka kufanikisha hatua ya kupata njia salama katika kivuko cha Rafah, ili kupitisha misaada kuingia Ukanda wa Gaza, baada ya Israel kuamuru kuzingirwa kwa ukanda huo.Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekanusha taarifa za usitishwaji mapigano na Hamas.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!